Professional Documents
Culture Documents
OLOKUN
OLOKUN
Awali ya yote napenda kuwakumbusha wale wanaotaka utajiri juu ya pete na mafuta ya mami
wata , kwa wale wanaotaka kusafisha njia zao za kipato na kujiondolea vifungo vya kimaisha
pamoja na kung’arisha nyota zao usipitwe na mafuta ya awla bulbul, kwa wale wenye kuhitaji
elimu za tiba asili na kufahamu mambo yanayofanyika katika ulimwengu wa siri usithubutu
kupitwa na vitabu vya Maalim shafii the don.
kuwasiliana na Maalim shafii the don usisite kumpigia simu katika nambari yake inayoanza na
+255 692 007 575. Karibu
Olokun ndiye mtawala wa maji na roho wote wa majini, ana mamlaka juu ya vyote vilivyo
ndani na karibu ya maji. Mwenye uwezo wa kutoa mali, afya, na ustawi wa kila nyanja. Olokun
ni Orisha au roho yenye uungu inayosimamia kuingiza roho ulimwenguni na kuziongoza katika
maisha ya baada ya kifo.
Pia anajulikana kama jini wa kifalme mwenye utajiri mkubwa na ana baraza la majini
wanaomshauri akiwemo yemaya , mami wata na oshun ambao mara nyingi hufanya kazi kama
mawaziri wake, Wafuasi wa Olokun wanaamini kuwa roho huyo anaishi chini kabisa ya bahari
mahala ambako hata mwanga wa jua haupenyezi
Olokun huoneshwa kama samaki mtu na wakati mwingine jinsia yake huwa ni tata, wapo
wanaoamini ni mwanamke na wapo wanaoamini ni mwanaume, huenda hii ni kwasababu mara
nyingi humtumia mke wake yemaya kumuwakilisha katika kazi zake, ni jini msiri na asiye
patikana kirahisi rahisi hivyo wengi hawamjui vyema,
kama kila Orisha , Olokun ana asili ya duality yaani uwili ~ anajulikana kama chanzo cha
uzaliwaji wa viumbe hai vyote ikiwemo mimea, na pia anajulikana kama mwenye mamlaka ya
ulimwengu wa wafu. Kama ilivyo kwa dunia, wayoruba walikuwa wakiamini kuwa vitu vingi
asili yake ni baharini na hata mwisho wake kuishia baharini , wayoruba wanaamini pia Mungu
alipoiumba bahari , papo hapo akatokea na mmiliki wa bahari ama kwa jina la kiyoruba Olokun
ambae hasira yake juu ya matendo ya binadamu ndio hupelekea kutokea kwa tsunami.
wanasayansi wa hivi sasa wanaamini kuwa viumbe hai wa kwanza kabla ya binadamu viliibuka
kutokea baharini , majibu ya tafiti zao yanazua mafumbo mengi zaidi na kuwalazimisha
wanasayansi wazidi kutafiti siri za bahari.
Kwa maana hiyohiyo hata binadamu anazaliwa kutoka kwenye tumbo la mama na ndani ya
mfuko wa ujauzito kuna kioevu amniotic au amniotic fluid , majimaji yenye chumvi
yanayomzunguka mtoto na kulinda ukuaji wake hadi kuzaliwa hilo linafanya maji na chumvi
yaonekane kuwa na nguvu ya uumbaji na binadamu ana mahusiano na bahari.
Wayoruba wanaamini chini ya kina cha bahari, lipo eneo ambalo roho ya binadamu ni lazima
ivuke baada ya kufa au kabla ya kuzaliwa, imani hiyo inafanana na imani ya wachina juu ya mto
wa wang chuan uliopo katika ulimwengu wa kiroho, Wayoruba wanaamini Olokun ndio mwenye
mamlaka ya ulimwengu huo.
Wayoruba wanaamini kuwa baada ya Mungu kuumba kila kitu, miungu mingi iliishi mbinguni
lakini Olokun hakuwahi kuiacha bahari na kutimiza majukumu yote aliyopangiwa hivyo Mungu
muumba akampa mamlaka ya juu zaidi kwa baharini kuliko Orisha mwingine yoyote.
Kwakuwa utajiri wa dunia ni sawa na punje ya mchele ukilinganisha na utajiri uliopo
baharini,Olokun anafahamika kama Mungu mkuu wa utajiri kwa tamaduni nyingi za kiafrika na
watu wa jamii tofauti ikiwemo Cuba hufanya maagano na Olokun pamoja na kuvaa Vidani vya
cheni , pete na bangili zilizotengenezwa kwa nishati na roho ya Olokun ili kuvuta utajiri wa
bahari.
Olokun anaonekana kama mmoja wa Waorisha waliostahimili zaidi katika dini ya Kiyoruba,
Olokun ana mtoto ambaye pia ni mungu wa utajiri mwenye kufanya kazi badala ya baba yake,
naye anaitwa Aje Olokun. Roho wote wenye asili ya uzao wa Olokun hawatambulikagi jinsia
kwasababu wanaweza chukua umbile lolote wanalolitaka, hata baba yao Olokun akitokea katika
umbile halisi huvaa vazi lenye rangi za bluu za aina tisa kama samawati,samawati ya
kigiza,samawati ya kifalme,aguamarine nakadharika, kwa ujumla zipo aina 50 za rangi za bluu,
vazi hilo alivaalo Olokun huficha umbile lake na usoni huvaa kinyago , pia Olokun huvaa
mkufu wenye shanga ambao una matumbawe na rangi ya maziwa , kijani kibichi na bluu
iliyokolea. Nambari zake ni saba na tisa.
Wazaliwa wote wa Olokun pia ni Wamiliki wa utajiri wa baharini. Wanaishi kwenye kina kirefu
cha bahari, mahala penye furaha kubwa . Olokun ni Orisha mwenye shauku na amri , ana sifa ya
uvumilivu, nguvu, hasira na hekima, wafuasi wanaomjumuisha Olokun katika maombi yao,
hupewa ulinzi na mwongozo wa kimaisha
Maalim Shafii the don anasema ukimuita Orisha huyu na kufanya naye maagano basi unatakiwa
kujua kuwa sadaka zake hupelekwa baharini kila mwaka . Watu humuita na kuomba ujuzi wa
mambo, kupata afya kutokana na magonjwa, kupata baraka, utajiri nakadharika. Sadaka
anazopendelea ni bukini wanaofanana na bata maji ,bata wa kawaida, njiwa, kanga , nguruwe, na
jogoo lakini pia unaweza kumuahidi unachoweza kukitoa kama sadaka sharti utimize
unachokiapia . Roho wote wa uzao wa Olokun Wanapenda matunda ya aina zote hasa matikiti
pamoja na chakula cha viazi vikuu vilivyopikwa. Maalim anasema ukipewa utajiri wa Olokun
unatakiwa kutimiza ahadi utakazoapa kumpa kama sadaka, kama hutotimiza ahadi yako unaweza
kwenda na maji
Njia nyingine ya kumwita Olokun ni kutandaza leso nyeupe kwenye madhabahu yako. Kisha
weka mdoli wa Olokun au sanamu kwenye leso. Maalim anasema utaweka na unga wa uvumba
wa Yemaya, unga wenye maajabu kwelikweli, kisha unga huo utie kwenye mkaa na uwashe.
Mara tu uvumba ukiwashwa, unaweza kuanza kutoa sadaka yako kwa Olokun.
Maalim pia anasema ukiwa na pete ya Olokun halafu ukiwa na uvumba wa yemaya unaweza
kufanya mambo ya ajabu kwelikweli ila hiyo ni mada ya siku nyingine.
Mara nyingi matambiko ya Olokun hufanyika kila mwaka , sanasana huko nchini Nigeria
pamoja na nchi zenye dini ya Kiyoruba.mfano katika Jimbo la Lagos, hufanya sherehe za
Olokun katika mwezi wa Novemba. Ukienda Edos, katika mji Usonigbe utakuta hekalu kubwa
la Olokun, wao husherehekea na kufanya ibada kuu za Olokun mwishoni mwa mwezi wa
Februari.
Na huu ndio mwisho wa darasa la Maalim shafii the don