You are on page 1of 2

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Simu: +255-22-2700493…6 S.L.P. 2624 or 32019


+255-22-2700499 DAR-ES-SALAAM
+255-22-2772423
Fax: +255-22-2775966
E-mail: esnecta@necta.go.tz

Toleo la Mei, 2019 MM1


FOMU YA MAOMBI YA MAREKEBISHO YA MAJINA

A. MAELEKEZO MUHIMU:
i. Jaza taarifa sahihi kwa kila nafasi iliyoachwa wazi.
ii. Marekebisho ya majina katika vyeti hufanyika katika kipindi cha mwaka mmoja tangu
kusambazwa kwa vyeti.
iii. Iwapo ni mtahiniwa wa kujitegemea, baada ya kubaini kosa katika uandishi wa jina lako
wasiliana na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa kuandika barua kwenda kwa
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania.
iv. Iwapo ni mtahiniwa wa shule, wasiliana na Mkuu wa shule uliyofanyia mtihani ili
athibitishe marekebisho ya jina hilo kwa kuambatanisha nakala ya fomu ya usajili wako.
Kielelezo hicho kiambatanishwe kwenye barua yako ya ombi la marekebisho ya jina na
kuvituma kwa kutumia anwani ifuatayo: Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la
Tanzania S.L.P. 2624 Dar es Salaam.
v. Barua (kwa watahiniwa wa shule na kujitegemea) hiyo ioneshe jina, namba ya mtihani,
aina ya mtihani, mwaka na shule au kituo ulichofanyia mtihani na kueleza jina lenye
makosa na jina sahihi.
vi. Vyeti vilivyokosewa majina virudishwe NECTA.
vii. Baada ya uchunguzi kukamilika, iwapo itabainika kuwa kosa halikusababishwa na NECTA,
utatakiwa kulipa Tshs. 35,000/= za marekebisho ya jina.
viii. Malipo yanapaswa kufanyika kwa kutumia namba maalum (Control Number) inayotolewa
na mfumo wa malipo ya serikali wa kielektroniki (GePG) kupitia tovuti ya NECTA:
www.necta.go.tz. Malipo yote yafanyike katika benki za: -NMB; CRDB na NBC au kwa
kutumia mitandao ya kifedha ya M-Pesa na Tigo Pesa.
ix. Baada ya malipo kufanyika, Risiti halisi ya malipo na fomu ya marekebisho ya majina (print
kutoka kwenye mtandao wa NECTA: www.necta.go.tz) iliyojazwa vitumwe NECTA.
x. Marekebisho yakishafanyika, Results Slip au cheti chenye jina sahihi kitatumwa kwako
kupitia anwani inayohusika (anwani zao kwa watahiniwa wa kujitegemea au kwa anwani za
shule kwa watahiniwa wa shule).

Barua zote zielekezwe kwa Katibu Mtendaji


B. TAARIFA ZA MTAHINIWA

Jina la mtahiniwa………………………………………………………………………………
a) Namba ya mtihani………………………………………………………......
b) Mwaka wa mtihani……………………………………………….............
c) Aina ya mtihani: (CSEE, ACSEE, DSEE, GATCE, GATSCCE, DTE, PSLE)………………………
d) Jina lililokosewa………………………………………………………………..
e) Jina lilivyostahili kuandikwa………………………………………………
f) Namba ya simu ya mkononi………………………………………………
g) Anwani ya mtahiniwa………………………………………………………..
h) E-mail ya mtahiniwa………………………………………………………….
i) Saini……………………………….Tarehe………………………………………

You might also like