You are on page 1of 2

Benki ya CRDB, IFC zakubaliana maeneo sita ya ushirikiano

Washington US 15 Desemba 2022 - Benki ya CRDB na Shirika la Kimataifa la Fedha la Benki


ya Dunia (IFC) wamekubaliana maeneo sita mahususi ya ushirikiano katika juhudi zao za
pamoja za kukuza ujumuishi wa kifedha nchini Tanzania na ukanda mzima wa Afrika
Mashariki.

Makubaliano hayo yamefikiwa na ndio watendaji wakuu wa taasisi hizo mbili wakati wa
mkutano wao huko Washington uluofanyika sambamba na Mkutano wa Wakuu wa nchi za
Afrika na Marekani.

Katika mkutano huo, ujumbe wa Benki ya CRDB uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dk Ally
Laay, Makamu mwenyekiti, Prof Neema Mori, na Mkurugenzi Mtendaji wa Group, Abdulmajid
Nsekela, huku IFC ikiwakilishwa na Mkurugenzi anayesimamia ushirikiano na Taasisi za Fedha
Duniani, Tomasz Telma.

IFC ni mshirika wa muda mrefu na wa kimkakati wa Benki ya CRDB na imekuwa na jukumu


muhimu katika kusaidia mkakati wa benki tangu 2014.

“IFC imekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Benki ya CRDB katika kipindi cha
miaka minane iliyopita na katika kufanikisha utekelezaji wa mkakati wetu wa miaka mitano
ambao unamalizika mwaka huu,” alisema Nsekela katika taarifa yake iliyowasilishwa kwa
vyombo vya habari jijini siku ya Jumatano.

Alisema mkutano wa Washington ulilenga kuwaleta pamoja viongozi wakuu wa taasisi hizo
mbili ili kujadili maeneo ya ushirikiano na uungaji mkono.

“Tumekubaliana kushirikiana katika masuala yanayohusu ufadhili wa shughuli za wanawake na


vijana; ufadhili wa miundombinu nchini Tanzania, Burundi na DRC, pamoja na kusaidia upanuzi
wa huduma za Benki yetu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini,” Bw Nsekela alisema.

Taasisi hizo mbili, alisema pia zilikubaliana kushirikiana katika ufadhili wa miradi ya mazingira,
kilimo biashara, pamoja na kuijengea uwezo Benki ya CRDB katika kubuni na kusimamia
miradi ya ufadhili kiuchumi.

Katika maelezo yake wakati wa mkutano huo, Telma alielezea kwa kina uzoefu wa IFC katika
kufadhili miradi nchini Tanzania na akabainisha kuwa nchi ina fursa nyingi za kiuchumi, huku
akipongeza jitihada zinazofanywa na serikali katika kufungua uchumi.

Alieleza kwa kina uhusiano wa IFC na Benki ya CRDB, na kuipongeza benki hiyo kwa utendaji
mzuri kulinganisha na taasisi nyengine za kifedha.
Telma alisema kwa kuwa IFC na Benki ya CRDB wamekuwa wakifanya kazi pamoja kwa miaka
mingi, ana matumaini kuwa majadiliano hayo yatafungua fursa mpya za ushirikiano zaidi kati
ya taasisi hizo mbili.

Katika mada yake katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela alieleza kuwa Benki ya CRDB ina mizania ya Sh10.9 trilioni na mtaji wa Sh1.4 trilioni.
Benkin hiyo hiyo pia inajivunia kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia njia
mbadala na kuchochea ukuaji wa kiuchumi.

Ikiwa na CRDB Wakala zaidi ya 25,000, na huduma mdadala za kidijitali ikiwamo SimBanking,
SimAccount, pamoja na ATM za kubadilisha fedha, asilimia 93 ya miamala ya Benki ya CRDB
inafanyika nje ya tawi.
Kutokana na ufanisi huo, mwaka 2021 faida halisi ya Benki ya CRDB ilipanda hadi Sh268 bilioni
kutoka Sh36 bilioni pekee mwaka 2017 huku faida ya jumla ya miezi tisa ya kwanza ya mwaka
huu 2022 wa ikifika Sh257 bilioni.
Benki hiyo imerekodi amana za Sh7.672 trilioni hadi robo ya tatu ya 2022, kutoka Sh4.326
trilioni zilizosajiliwa mwishoni mwa 2017. Vile vile, Benki ya CRDB ilikuwa imefanya uwezeshaji
wa mikopo ya jumla ya Sh6.244 hadi kufikia Septemba 30, 2022, kutoka Sh2.894 trilioni
mwishoni mwa 2017.
Aidha, Mapato ya Mtaji yameimarika kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita, benki pia imeweza kudhibiti viwango vya Mikopo Chechefu, Uwiano wa Gharama kwa
Mapato kufikia viwango vinavyohitajika na Benki Kuu ya Tanzania.
Wakati matayarisho ya utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano ijayo (2023 hadi 2027)
yakiendelea, Nsekela amesema matarajio ya benki hiyo ni kwamba miaka mitano ijayo
itashuhudia kipindi kingine cha ukuaji katika viashiria vyote muhimu vya utendaji.
“Tumetumia miaka 5 iliyopita kuboresha mifumo yetu ya utendaji na utuaji huduma kwa
wateja, lakini pia tumejenga msingi sahihi wa kukuza biashara na kuongeza thamani kwa
wadau wetu. Mkakati huu mpya unasisitiza katika kuijenga Benki bora zaidi kiutendaji na
kuwekeza katika ubunifu wa huduma na bidhaa tukilenga kuboresha maisha ya watu na
uchumi kwa ujumla,” alisema.

You might also like