You are on page 1of 96

FASIHI

KARIBU KWENYE DARASA LA FASIHI

YALIYOMO

 MAANA YA FASIH NA UCHAMBUZI WA VIPERA

 MAANA NA METHALI ZILIZOKUSANYWA

 FILAMU NI SEHEMU YA FASIHI YA KISWAHILI

MAANA YA FASIHI NA UCHAMBUZI WA VIPERA VYAKE

Williady, (2015) Fasihi ni tawi moja wapo la sanaa linalotumia lugha katika
kuwasilisha ujumbe wa mdomo au wa maandishi.

Wamitila (2004) Fasihi ni sanaa inayotumia luha na ambayo hujishughulisha na


binadamu pamoja na maisha yake na huathri, hugusa au huacha athari fulanina
hupatikana katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii Fulani.

Kwakuwa fasihi ni aina ya sanaa, ni vyema mwanafunzi akajua pia maana ya


sanaa.

MAANA YA SANAA

(Williady: 2015) Sanaa ni ujuzi au ufundi wenye kuleta manufaa kwa uma.

UMBO LA SANAA

Tunaposema umbo la sanaa tunamaanisha matawi yanayojenga sanaa. Matawi


hayo nipamoja na;

Fasihi, maonyesho, ususi, uhunzi, ufumaji, utarizi, uchongaji, ufinyanzi,


uchoraji na muziki.
AINA/ KUMBO/ TANZU ZA FASIHI
Katika kumbo ya fasihi na taaluma zake kuna aina kuu mbili za fasihi, ambazo
ni;

Fasihi Simulizi

Fasihi Andishi

TOFAUTI KATI YA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI

Namna ya uwasilishaji wake. Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia yam domo
wakati fasihi andishi uwasilishwa kwa njia ya maandishi.

Mabadiliko. Fasihi simulizi huweza kupokea mabadiliko ya papo kwa papo


wakati fasihi andishi hurekebishwa baada ya toleo jipya.

Utendaji wake kwa hadhira na fanani. Hadhira na fanani katika fasihi


simulizi huwa ni yakiutendaji, wasikilizaji wanaweza kuchangia mawazo kwa
kutoa maoni, kuuliza maswali au kushadadia masimulizi ya fanani. Fasihi
andishi hadhira hawawezi kuchangia lolote.

Ukongwe. Fasihi simulizi niyazamani zaidi, ilianza wakati mwanadamu


alipoanza kutumia mdomo katika mawasiliano. Fasihi andishi ilianza pindi
maandishi yalipobuniwa.

Vidato na elimu. Fasihi simulizi haiitaji mtu ajue kusoma ama kuandika,
inamuhitaji mtu mwenye uwezo wa kuzungumza. Fasihi andishi inamhitaji mtu
anayejua kuandika na kusoma.

Umiliki. Fasihi simulizi inamilikiwa na jamii nzima wakati fasihi andishi


humilikiwa na mwandishi aliyeandika na kupiga chapa kazi hiyo.

Idadi ya tanzu. Fasihi simulizi inatanzu nyingi zaidi kuliko fasihi andishi.
Kuhifadhi. Hapo kale fasihi simulizi ilihifadhiwa kichwani, kwa sasa
fasihi simulizi yaweza kuhifadhiwa katika vinasa sauti, kaseti na santuri. Fasihi
andishi yenyewe huifadhi wake ni kwa njia ya maandishi.

Mwingiliano wa tanzu kwa kiasi. Fasihi simulizi huweza kuingiliwa kwa


kiasi kikubwa na tanzu nzingine kama vile methali, vitendawili, nyimbo na
nahau wakati fasihi andishi huweza kuingiliwa na tanzu nyingine kwa kiasi
kidogo.

UFAFANUZI WA AINA ZA FASIHI

1.Fasihi simulizi

Fasihi simulizi ni aina ya fasihi inayotumia mdomo na utendaji wa viungo vya


mwili katika kuwasilisha maudhui ya fanani kwa hadhira iliyokusudiwa.

TANZU ZA FASIHI SIMULIZI

Hadithi, uigizaji, ushairi na semi

VIPERA VYA HADIDHI

Ngano, vigano, hekaya, soga, tarihi, visa, visasili, shajara, istiala, michapo
na mbazi

VIPERA VYA UIGIZAJI

Miviga, michezo ya jukwaani, majigambo, utani, vichekesho, ngonjera,


mgomezi na mazungumzo

VIPERA VYA USHAIRI

Nyimbo, maghani, ngonjera, mashairi, tenzi na tendi

AINA ZA NYIMBO
Bembezi, nyimbo za mapenzi, nyiso, nyimbo za jadi, nyimbo za harusi, nyimbo
za watoto nyimbo za sifa, nyimbo za kampeni, nyimbo za maombolezo na
nyimbo za chombezi.

VIPERA VYA SEMI

Methali, misimu, lakabu, nahau, vitendawili. utani, misimu, mafumbo,


masaguo, mizungu na misemo

MAJUKUMU / DHIMA ZA FASIHI SIMULIZI KATIKA JAMII

Kuelimisha, kuburudisha, kusisimua, ukombozi, kutoa mwongozo kwa jamii,


kutunza amali
za jamii (historia na utamaduni), kujuza na kuunganisha vizazi nz
vizazi, kufundisha,
kudumisha uhusiano, kudumisha ushirikiano na kukuza stadi za lugha

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA USIMULIZI


WA HADITHI

Ili msimuliaji aweze kutongoa au kusimulia hadithi kwa usahihi inampasa


awe na weledi wa kutosha juu ya mbinu za kusimulia hadithi. Mbinu hozo
ni hizi;

A) Dhima na maudhui

Msimuliaji wa hadithi anapaswa kujua lengo kuu (dhima) la hadithi yake.


Vilevile msimuliaji anapaswa kujua maudhui ambayo ni jumla ya mambo
yote yanayopelekea hadithi kutiririka vizuri kwenye mkondo wake.
B) Msuko

Msuko wa matukio kwa jina jingine unafahamika kama muundo.


Kipengele hiki cha muundo kinahusu mpangilio wa hadithi kuanzia
mwanzo mpaka mwisho.

C) Kusisimua

Kusisimua ni mbinu inayovuta umakini kwa watu. Msimuliaji anaweza


kutumia mbinu kadhaa zitakazo msisimusha msomaji, mbinu kama vile
taharuki, miguno na kelele za kutisha.

D) Urudufishaji

Huu ni urudiaji rudiaji katika fasihi simulizi. Mara nyingi msimuliaji


anashauriwa kurudia rudia maneno, falsafa, nahau au vitendawili
vilivyobeba lengo kuu la hadithi yake.

E) Chombezo

Chombezo ni kipengele kidogo kinacho elezwa na mtambaji wa hadithi


chenye lengo la kupunguza ukakasi ama ukalia ama vitisho vilivyotokana
na maudhui ya hadithi Fulani.

F) Nyimbo
Nyimbo zina kazi nyingi katika masimulizi ya hadithi. Moja wapo ya
matumizi hayo ni kama vile kuondoa uchovu kwa wasikilizaji, kuvuta
usikivu, kuwakaririsha hadhira falsafa au lengo kuu la hadithi hiyo.

MAMBO MENGINE

a) Utulivu kwa hadhira

b) Ujenzi wa wahusika

c) Matumizi ya tamathali za semi

d) Ujenzi wa taswira

2. FASIHI ANDISHI

Williady (2015) fasihi andishi ni aina ya fasihi inayowasilishwa kwa ustadi


wa maandishi yenye kuleta maana.

Wamitila (2004) fasihi andishi ni sanaa inayowasilishwa kwetu kwa


maandishi.

TANZU ZA FASIHI ANDISHI

RIWAYA (NATHARI)

USHAIRI (NUDHUMU)

TAMTHILIYA (SANAA ZA MAONYESHO)

FANI NA MAUDHUI KATIKA FASIHI

Fani na maudhui katika fasihi ndio maumbo mawili makuu yanayobeba


sanaa hii.

FANI
Fani ni ufundi unaotumiwa na msanii katika kufikisha ujumbe
uliokusudiwa, fani sio ujumbe bali ni mfano wa kipaza sauti kinachotumika
kufikisha ujumbe.

VIPENGELE VYA FANI

Fani inavipengele vingi, kila kipengele kina husika kipekee kwa


kutofautiana na kipengele kingine.

Vipengele vya fani ni pamoja na;

a) Muundo

Kipengele hiki hutumiwa kueleza mpangilio wa kazi ya kifasihi. Kwa ufupi


kwenye kipengele cha muundo tunaangalia umbo la kazi ya fasihi, mfano
kazi yaweza kugawanywa katika sura mbalimbali, sura hizi ndizo ujenga
muundo.

b) Mtindo

Williady (2015) mtindo ni mbinu za kipekee zinazomtofautisha msanii


mmoja na mwingine. Mfano katika fasihi simulizi kipengele cha nyimbo
hadhira inaweza kusikia wimbo kwa mara ya kwanza na kutambua wimbo
huo umeimbwa na nani bila ya kuambiwa na mtangazaji, hii huweza
kutokea pindi mwimbaji mashuhuri anayetumia mtindo wa peke yake
katika sauti na mpangilio wa mashairi anapotoa wimbo mpya. Huu ndio
huitwa mtindo. Katika fasihi andishi mtindo unaweza kujitokeza kwa njia
za kipekee za mtunzi katika matumizi ya lugha, methali na misemo, msuko
na mpangilio wa vina na mizani katika ushairi.

c) Mandhari

Williady (2015) Mandhari ni eneo au mazingira ya kweli au yakubuni


ambayo hutumiwa na mwandishi katika kuwajenga wahusika na uhusika
wao.
d) Matumizi ya Lugha

Williady (2015) Matumizi ya lugha ni ustadi wa msanii katika kutumia


lugha itakayoleta mvuto kwa wasomaji au wasikilizaji wa kazi ya fasihi.

Katika kutumia lugha msanii lazima azingatie kipengele cha uteuzi wa


maneno yanayoendana na hadhira yake, maneno hayo ndiyo yatakayoleta
mfungamanisho katika ya msanii, hadhira na ujumbe uliokusudiwa.

e) Matumizi ya tamathali za
semi(usemi)

Williady (2015) Tamathali maanayake ni neon moja au kifungu cha maneno


kilicho sukwasukwa na kufichwa maana.

Baadhi ya tamathali za semi katika Kiswahili ni pamoja na;

Tashibiha, sitiari, tafsida, tashihisi, chuku, kinaya,dhihaka,


mbalagha,tabaini

f) Mbinu nyingine za kisanaa

Hapa huwa na mchanganyiko wa mbinu kadhaa katika usimulizi na


silazima mbinu hizo zitumike zote kwa wakati mmoja. Mfano wa mbinu
hizo ni pamoja na;
Takriri, kuchanganya ndimi, tanakali sauti, taswira, lakabu, nahau na
misemo

e) Wahusika

Williady (2015) wahusika ni viumbe hai au viumbe ambao si hai


wanaobebeshwa majukumu na msanii ili kuwafikishia hadhira ujumbe
uliokusudiwa.

MAUDHUI KATIKA FASIHI SIMULIZI

(williady: 2015) Maudhui ni jumla ya mawazo anayoyazungumzia msanii


au mtunzi katika kazi ya fasihi.

Maudhui hujumuisha vipengele mbalimbali, kama vile;Dhamira, ujumbe,


falsafa, mafunzo, migogoro na mtazamo.

TANBIHI: Kuna baadhi ya wataalamu wa lugha wanakiweka kipengele cha


migogoro upande wa fani na kunabaadhi wanakiweka kipengele hiki
upande wa maudhui. Mimi nakiweka upande wa maudhui kwa kuwa
migogoro inabeba kwa kiasi kikubwa ujumbe kuliko ufundi.

DHAMIRA

Dhamira ni shabaha kuu ya mtunzi wa kazi ya fasihi. Shabaha hii


ukusudiwa ni nani wakumlenga nayo. Msanii anaweza kuwalenga
kimaudhui watoto, wanawake, wasomi au watu wote katika jamii. Shabaha
hii yaweza kuandikwa au kutongolewa kwa mdomo ikiwa na lengo la
kupongeza, kuhimiza, kushauri, kutoa taarifa na kukosoa.

UJUMBE

Ujumbe ni mawazo yanayotokana na dhamira, mawazo haya yaweza


kujitokeza waziwazi au kwa kificho.

FALSAFA

Falsafa ni hekima hekima ya mtunzi. Mtunzi huamini kuwa kupitia imani


hii jamii inaweza kupata suluhisho la matatizo yanayowakabili. Kwa mfano
shekhe Shaaban Robert aliamini kuwa kila mwanajamii akiwa na utu basi
haki na upendo vitapatikana kirahisi.

MAFUNZO

Mafunzo ni nasaha anazotoa mtunzi ambazo huifundisha hadhira maadili


Fulani. Maana ya mafunzo hutegemea namna hadhira inavyofasili nasaha
hizo.

MIGOGORO

Migogoro ni misuguano au mikinzano ama kutoelewana kati ya pande


mbili au zaidi ndani ya kazi za fasihi.
AINA ZA MIGOGORO

Mgogoro kati ya mtu na mtu

Mgogoro kati ya mtu na jamii

Mgogoro kati ya jamii na jamii

Mgogoro wa nafsi

VI. MTAZAMO

Mtazamo na jinsi mwandisi anavyotazama na kuyachukulia matukio katika


ulimwengu na athari zake kwa wanajamii. Mfano waandishi wengi wa
mashairi wanamtazamoa huu “Kuibuka kwa maovu mengi duniani
kwasasa ni matokeo ya binadamu kuasi dini.

METHALI ZA KISWAHILI

ZIMEKUSANYWA NA MWL. MAJUMBENI

Methali ni nyenzo ya msingi katika makuzi ya fasihi ya Kiswahili. Tangu


kale Methali zimetumika katika kujenda jamii kwa kutoa maonyo na
kuambukika tabia njema hasa kwa vijana wanaochipukia.

Wataalamu wengi wameeleza maana ya Methali, lakini maana halisi bado


inaendelea kushabihiana japokuwa kuna mikinzano katika baadhi ya
maeneo. Maana halisi ya methali itabaki kuwa,
“Methali ni kipera cha semi katika fasihi simulizi kinachojengwa kwa
pande mbili, pande moja ni yenye kuuliza swali na nyingine yenye kujibu
swali zikiwa na lengo la kufunza amali za jamii kwa vijana.

Mwl. Majumbeni amekusanya methali nyingi katika lugha ya Kiswahili,


baadhi ya methali ameziweka humu kwenye blogi yake kwa lengo la kutoa
mchango wake katika ukuzaji na uendeshaji wa shughuli zote zinazohusu
lugha ya Kiswahili.

Zifuatavyo ni baadhi ya METHALI , zikiwa vimepangwa ki - alfabeti:

“A”

1. Adhabu ya kaburi aijua maiti

2. Adui mpende

3. Aibu ya maiti aijua mwosha

4. Aisifuye mvua imemnyea

5. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke

6. Achambaye na gunzi hatakatiki

7. Akimbiaye mvua, akimbia shibe

8. Akiba haiozi

9. Akili ni mali

10. Akili ni nywele kila mtu ana zake


11. Akili nyingi huondoa maharifa

12. Akipenda chongo, huita kengeza

13. Akumulikaye mchana, usiku akuchoma

14. Akutendaye mtende mche asiyekutenda

15. Anaekula kibudu, ashibisha tumbo wala si nafsi

16. Alalaye usimwamshe, ukimwamsha utalala wewe

17. Alisifiye jua, limemwangaza

18. Aliye kando haangukiwa na mti.

19. Aliyekupa wewe kiti, ndiye aliyenipa mimi kumbi

20. Aliyetota, hajui kutota

21. Amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga

22. Amnyimaye punda adesi, kampunguzia mashuzi

23. Ana hasira za mkizi

24. Anayekataa wengi ni mchawi

25. Amtukanaye jumbe hafikwi na kesi

26. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi na kuaga

27. Anayeonja asali, huchonga mzinga

28. Anayetaka hachoki hata akichoka keshapata

29. Angakaanga, tu chini agae

30. Angenda juu kipanga, hafiki mbinguni

31. Angurumapo simba, mcheza nani?

32. Aninyimaye mbaazi, kanifunguzia mashuzi


33. Atupaye kopo la choo, hafikwi na haja

34. Apewaye ndie aongezwaye

35. Asiye bahati habahatiki / habahatishi

36. Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu

37. Asiyejua jua maana, haambiwi maana

38. Asiyekujua hakudhamini

39. Asiyekubalikushindwa si mshindani

40. Asiyekuwapo machoni, na moyoni hayupo

41. Asiyekuwapo na lake halipo

42. Asiye na mengi, ana machache

43. Asiye na meno, hapewi nyama ya kiuno

44. Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu

45. Asiyeuliza, hanalo ajifunzalo

46. Atangaye sana na jua, hujua

47. Atangazaye mirimo si mwana wa ruwari

48. Auguwaye, huangaliwa

49. Avuaye nguo, huchutama

50. Avumaye bahariki papa (kumbe wengine wapo)

“B”

51. Baada ya dhiki, faraja

52. Baada ya kisa, mkasa


53. Baada ya chanzo, kitendo

54. Baba wa kambo si baba

55. Bandu! Bandu! Huisha gogo

56. Baniani mbaya, kiatu chake dawa

57. Bendera hufuata upepo

58. Bembea umpa raha apendae

59. Bilisi wa mtu ni mtu

60. Bura yangu sibadili na rehani

“C”

61. Cha mlevi huliwa na mgema

62. Chanda chema huvikwa pete

63. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza

64. Chombo cha kuzama hakina usukani

65. Chombo kilichopikiwa samaki, hakiachi kunuka vumba

66. Chovya – chovya! Yamaliza buyu la asali

67. Chururu si ndo!ndo !ndo

68. Dalili ya mvua ni mawingu

69. Damu nzito kuliko maji

70. Dau la mnyonge halendi joshi

71. Dawa ya moto ni moto

72. Debe tupu haliachi kuvunda


73. Dua la kuku halimpati mwewe

74. Dua mbaya haombolezewi mtoto

“E”

75. Elimu ni bahari

76. Ellimu ni ufunguo, haina mwisho

77. Elimu ya mjinga ni majungu

“F”

78. Fadhili za punda, mashuzi, na msihadhari ni ng’ombe

79. Fimbo iliyo mkononi, ndiyo iuayo nyoka

80. Fimbo ya mbali, haiui nyoka

81. Fuata nyuki, ule asali

82.Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu hulingamua

83. Fungato haliumizi kuni

84. Funika kombe mwanaharamu apite

“G”

85. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno

86. Gonga gogo usikilize mlio wake

87. Gonga! Gonga! utoka cheche


“H”

88. Haba na haba hujaza kibaba

89. Halla! Halla! Mti na macho

90. Hamadi, kibindoni, silaha, iliyo mkononi

91. Hamna! Hamna! Ndimo mlimo

92. Hapana marefu yasiyo na ncha

93. Hapana masika yasiyo na mbu

94. Hapana msiba usiokuwa na mwenziwe

95. Hapana siri ya watu wawili

96. Hapana ziada mbovu

97. Haraka haraka haina Baraka

98. Hasara humfika mwenye mabezo

99. Hasira, hasara

100. Hauchi – hauchi unakucha

101. Hayawi! Hayawi! Huwa

102. Heri kufa macho kuliko kufa moyo

103. Heri kufa mwili kuliko kufa roho

104. Heri kujikwaa dole, kuliko kujikwaa ulimi

105. Heri nusu ya shari kuliko shari kamili

106. Hewalla! Haigombi

107. Hiari yashinda utumwa


108. Hucheka kovu, asiyefikiwa na jeraha

109. Hakunyimae tonge, hakunyimi neon

“I”

110. Ihsani haiozi

111. Ikiwa hujui kufa, tazama kaburi

112. Iliyopita si ndwele, ganga ijayo

113. Ivushayo ni mbovu

114. Ivumayo haidumu ikidumu inamkono wa mtu

115. Iwapo nia, njia hupatikana

“J”

116. Jicho moja halizuii kutazama uchi

117. Jifya moja haliinjiki chungu

118. Jina jema hung’aa gizani

119. Jino la pembe si dawa yap ego

120. Jitihada haiondoi kudura

121. Jongoo hulia “uta wangu u kule”

122. Jogoo la shamba haliwiki mjini

123. Joka la mdimu linalinda watundao

124. Jungu bovu limekuwa magae


125. Jungu kuu halikosi ukoko

“K”

126. Kafiri akufaaye si Islamu asiyekufaa

127. Kamba hukatikia pembamba

128. Kanga moja, haistiri maungo

129. Kanga iliyotota, Uganda maungo

130. Kanga hazai ugenini

131. Kata pua, unga wajihi

132. Kawaida ni kama sheria

133. Kawia ufike

134. Kazi mbaya si mchezo mwema

135. Kelele za mlango haziniwasi usingizi

136. Kenda karibu na kumi

137. Kiburi si maungwana

138. Kichango, huchangizana

139. Kidole kimoja hakivunji chawa

140. Kiingiacho mjini si haramu

141. Kikulacho ki nguoni mwako

142. Kila chombo kwa wimbile

143. Kila mlango kwa ufunguo wake


144. Kila mtoto na koja lake

145. Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta kwake

146. Kila ndege huruka kwa bawa lake

147. Kilio huanza mfiwa, ndipo na wa mbali wakaingia

148. Kimya kingi kina mshindo

149. Kinga na kinga ndipo moto uwaka

150. Kinyozi hajinyoi na akijinyoa hujikata

151. Kinywa ni jumba la maneno

152. Kipendacho roho hula nyama mbichi

153. Kipendacho moyo ni dawa

154. Kipya kinyemi, ingawa kidonda

155. Kisebusebu na kiroho papo

156. Kisokula mlimwengu, sera nale

157. Kitanda usichokilala, hujui kunguni wake

158. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua

159. Kivuli cha mvumo huwafunika walio mbali

160. Kiwi cha Yule, ni chema cha Yule, hata ulimwengu wishe

161. Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza

162. Koko haidari mai

163. Konzi ya maji haifumbatiki

164. Kosa moja haliachi mke

165. Kozi mwana mandanda, kulala na njaa kupenda


166. Kuagiza, kufyekeza

167. Kuambiana kupo, kusikilizana hapana

168. Kucha Mungu si kilemba cheupe

169. Kuchamba kwingi kuondoka na mavi

170. Kufa kikondoo, ndiko kufa kiungwana

171. Kufa, kufaana

172. Kufa kwa jamaa, harusi

173. Kufa kwa mdomo, mate hutawanyika

174. Kuishi kwingi ni kuona mengi

175. Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele

176. Kukopa harusi, kulipa matanga

177. Kuku havunji yayile

178. Kuku mwenye watoto halengwi jiwe

179. Kula kutamu, kulima mavune

180. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana

181. Kulenga si kufuma

182. Kumla ngulu si kazi, kazi kumwosha

183. Kunako matanga, kumekufa mtu

184. Kunguru mwoga hukimbiza bawa lake

185. Kupanda mchongoma kushuka ngoma

186. Kupotea njia ndiko kujua njia

187. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri


188. Kutu kuu ni la mgeni

189. Kutwanga nisile unga, nazuia mchi wangu

190. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi

191. Kwa mwoga huenda kicheko kwa shujaa huenda kilio

192. Kwenda mbio si kufika

193. Kwenye miti hakuna wajenzi

“L”

194. La kuvuma halina ubani

195. La kuvunda halina ubani

196. Lake mtu halumtapishi bali humchefua

197. Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo

198. Liandikwalo ndilo liwalo

199. Lila na fila hazitangamani

200. Lipitalo, hupishwa

201. Lisemwalo lipo, ikiwa halipo, lipo nyuma linakuja

202. Lisilokuwepo moyoni halipo machoni

“M”

203. Maafuu hapatilizwi

204. Macho hayana pazia

205. Mafahali wawili hawakai zizi moja

206. Maiti haulizwi sanda

207. Maiti hachagui sanda


208. Maji hufuata mkondo

209. Maji huteremkia bondeni, hayapandi kilimani

210. Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga

211. Maji usiyofika hujui wingi wake

212. Maji ya kifuu ni bahari ya chungu

213. Maji yakimwagika hayazoleki

214. Majumba makubwa husitiri mambo

215. Majuto ni mjukuu, mwishowe huja kinyume

216. Mambo kikowa

217. Manahodha wengi chombo huenda mpera

218. Maneno mema humtoa nyoka pangoni

219. Maneno makali hayavunji mfupa

220. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika

221. Maskini akipata, matako hulia mbwata

222. Maskini na mwanawe, tajiri na mali yake

223. Mavi usiyala, wayawingiani kuku?

224. Mavi ya kale hayanuki

225. Mbaazi ukikosa maua, husingizia jua

226. Mbinu hufuata mwendo

227. Mbio za sakafuni, huishia ukingoni

228. Mbiu ya mgambo ikilia ina jambo

229. Mchagua jembe si mkulima


230. Mchagua nazi, hupata koroma

231. Mchakacho hujao, haulengwa na jiwe

232. Mchama ago hanye hanyeli, huenda akauya papo

233. Mchelea mwana kulia, hulia yeye

234. Mchele mmoja, mapishi mengi

235. Mcheka kilema hafi bila kumfika

236. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao

237. Mcheza kwao hutunzwa

238. Mcheza na tope humrukia

239. Mchimba kisima, hakatazwi maji

240. Mchimba kisima huingia mwenyewe

241. Mchimba kisima humtia mtuwe

242. Mchonga mwiko hukimbiza mikono yake

243. Mchovya asali hachovyi mara moja

244. Mchuma janga hula na wakwao

245. Mchumia juani hula kivulini

246. Mdharau mwiba mguu huota tende

247. Mdharau biu, hubiuka yeye

248. Meno ya mbwa hayaumani

249. Mfa maji hukamata maji

250. Mficha uchi hazai

251. Mfinyanzi hulia gaeni


252. Mfuata nyuki hakosi asali

253. Mfukuzwa kwao hana pa kwenda

254. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu

255. Mganga hajigangi

256. Mgema akisifiwa Tembo hulitia maji

257. Mgeni hachomi chaza mtaani akanuka

258. Mgeni ni kuku mweupe

259. Mgeni njoo mwenyeji apone

260. Mgonjwa haulizwi uji

261. Miye nyumba ya udogo, sihimili vishindo

262. Mja hana hiari

263. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi

264. Mkamia majihayanywi, akiyanywa humpalia

265. Mkata hana kinyongo

266. Mkata hapendi mwana

267. Mkate mkavu wa nyumbani ni bora kuliko nyama ya shuwa


yap engine

268. Mke ni nguo, mgomba kupalilia

269. Mkono mmoja hauchinji ng’ombe

270. Mkono mmoja haulei mwana

271. Mkono mtupu haulambwi

272. Mkono usioweza kuukata, ubusu


273. Mkosa kitoweo, humangilia

274. Kabuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu

275. Mkulima ni mmoja, walaji ni wengi

276. Mla cha mwenziwe na chake huliwa

277. Mla cha uchungu na tamu hakosi

278. Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekea

279. Mla mbuzi hulipa ng’ombe

280. Mla kwa miwili hana mwisho mwema

281. Mla, mla leo, mla jana kala nini?

282. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe

283. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye

284. Mlilala handingwadingwa, mwenye macho haambiwi tule

285. Mlimbua nchi ni mwananchi

286. Mnyamaa kadumbu

287. Mnywa maji kwa mkono mmoja, kiu yake I pale pale

288. Moja shika si kumi nenda uje

289. Moto hauzai moto

290. Mpanda farasi wawili, hupasuka msamba

291. Mpanda ovyo, hula ovyo

292. Mpemba akipata gogo, hanyi chini

293. Mpemba hakimbii mvua ndogo

294. Mpemba hashoni tomo dogo


295. Mpiga ngumi ukutani huumiza mkonoe

296. Mpofuka uzeeni hapotei njia

297. Msafuri kafiri

298. Msafiri maskani, ajapokuwa sultani

299. Msasi haogopi miiba

300. Msema pweke, hakosi

301. Mshare kwenda msituni haukupotea

302. Mshoni hachagui nguo

303. Msitukane wagema na ulevi ungalimo

304. Msitukane wakunga na uzazi ungalimo

305. Mstahimivu, hula mbivu

306. Mtaka cha uvunguni huinama

307. Mtaka nyingi nasaba hupata nwingi msiba

308. Mtaka nyingi faida husogeza nyingi hasara

309. Mtaka yote hukosa yote

310. Mtaka hunda haneni

311. Mtegemea nundu haachi kunona

312. Mtegemea ndugu hufa masikini

313. Mtembezi hula miguu yake

314. Mteuzi haishi tama

315. Mti hawendi ila kwa nyenzo

316. Mtondoo haufi maji


317. Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha mamaye

318. Mtoto akililia wembe mpe

Hizo ni baadhi ya methali zilizokusanywa na mwl. Majummbeni .

Kama wewe ni mtafiti au mdau wa Kiswahili unataka kujua kuhusu


methali au unahitaji methali vingi zaidi kwa matumizi ya kufundishia au
kuandika tasnifu, tafadhali wasiliana nami kwa,

0762 – 957493

0768 – 625660

hwilliady@ymail.com

majumbeni@gmail.com

FILAMU NI SEHEMU YA FASIHI YA KISWAHILI


Historia ya Filamu Afrika
Barani Afrika sanaa ya filamu ilianza kuonekana kutoka kwa wakoloni, ambao
waliitumia kama zana ya kuwaelimishia Waafrika, lakini wakiamini kwamba
Waafrika hawakuwa na uwezo wa kutenganisha ukweli na uongo (Diawara
1992). Mtazamo huu kwa sasa umeshapitwa na wakati, kwani Waafrika
wamekwishaelimika kiasi cha kutosha kung’amua mambo mbalimbali
yanayoendelea kwenye jamii zao. Kwa ufupi, Waafrika wa sasa wamehamasika
tofauti na wale wa miaka ya ukoloni. Pia, si Waafrika wote ambao hawakuweza
kutenganisha ukweli na uongo, bali ni mtazamo au kasumba tu iliyojengwa na
wakoloni wakati huo ili kuwadharau Waafrika.

Ukadike (1994:1) anaeleza kuwa mwanzoni Waafrika hawakuweza kumiliki


filamu mpaka ilipofikia miaka ya 1960 ambapo nchi nyingi za Afrika zilikuwa
zikipata uhuru. Anaendelea kusema kuwa kutokana na wimbi hili la kujipatia
uhuru, mataifa ya Afrika kama vile Senegal, Mali, Burkina Faso, Nigeria na
Tanzania yalianza kuwa na mamlaka juu ya sanaa hii kwa kutengeneza filamu
zao wenyewe. Waandaaji wa filamu wa Afrika walibadili mwenendo wa filamu
kutoka ule wa wakoloni ambao ulikuwa na lengo la kuimarisha utawala wa
kikoloni na kueneza utamaduni wao. Hivyo wasanii wa Kiafrika wakaanza
kuitumia sanaa hii kama chombo muhimu katika mapambano ya kuudumisha
utamaduni wa Mwafrika. Walifanya hivi kwa kuchunguza kwa kina utamaduni
wa Afrika na kuanza kujenga upya pale ambapo ukoloni ulikuwa umedunisha na
kupotosha. Ukadike (1994:166) anaendelea kusema kuwa waandaaji hawa
walionyesha hamu ya kuwasiliana na jamii zao, kuamsha uelewa na kisha
kuhamasisha jamii zao kupambana na changamoto zinazowakabili.

Cham (1996) anaeleza kwamba, filamu za Kiafrika zimekuwa zikiendana na hali


halisi ya jamii za waandaaji wa filamu. Anasema pia kwamba waandaaji hawa
wamekuwa wakitumia filamu kama njia ya kusaidia jamii kuondokana na
mawazo ya kitumwa, na kukabiliana na changamoto zinazowakabili. Juhudi hizi
zinathibitishwa na mwandaaji wa filamu aitwaye Kabore (2000) anaposema
kuwa yeye kama msanii ana jukumu la msingi la kuyatilia maanani anayoshiriki,
kwa kuwa ana mizizi na historia ambayo imeungana na historia ya jamii yake.
Anaongeza kuwa daima anaiakisi hali hii kwenye filamu anazoandaa. Msimamo
huo wa Kabore unakuja kipindi ambacho waandaaji wa filamu wanaingiza
vionjo vya Kiafrika ili kuyalenga mambo muhimu yanayoendana na maisha ya
watu wa jamii husika. Historia hii fupi ya filamu Afrika katika utafiti huu
itasaidia katika kutoa picha na kuonyesha maendeleo na malengo halisi ya
filamu za Kiafrika. Waandishi waliozungumzia historia hii wanasisitiza kuwa
filamu za Kiafrika zinapaswa kuendana na maisha na hali halisi ya jamii husika
ili kuweza kuisaidia jamii hiyo.

Historia na Maendeleo ya Filamu Nchini Tanzania


Kwa mujibu wa Smyth (1983:129-143), filamu nchini Tanzania ni utanzu wa
fasihi ambao ulianzishwa kipindi cha wakoloni. Filamu chache zilizoanzishwa
wakati huo zilikuwa na lengo la kuendeleza utawala wa kikoloni na kueneza
utamaduni wao. Katika Afrika hakukuwa na sehemu yoyote ambapo
palianzishwa kiwanda cha utengenezaji filamu za hadithi ndefu za kifasihi, bali
filamu nyingi zilikuwa ni za makala za kuzungumzia matukio halisi. Katika
makoloni ya Waingereza, utengenezaji wa filamu za hadithi ndefu umekuwa na
mafanikio na kuenea Afrika Magharibi kuliko Afrika ya Kati na Afrika
Mashariki. Miongoni mwa sababu zilizokwamisha mafanikio ya utengenezaji
wa filamu za kifasihi ni kukosekana kwa mfumo wa kubadilisha fedha za kigeni,
udhibiti wa mgawanyo wa fedha hizo na ufinyu wa soko la taifa. Pia kushindwa
kwa serikali za Kiafrika kurudisha na kuzitumia fedha zilizopatikana kutokana
na kodi ya sinema katika uzalishaji wa ndani wa filamu.
Kwa mujibu wa Nottcut na Lathan (1937), sanaa ya filamu ilianza kuingia
nchini Tanzania miaka ya 1920. Kwa upande wa Tanzania maendeleo ya filamu
yalichochewa na nchi za Ulaya na za Kiafrika. Mwanzoni kabisa mwa miaka
ya 1920 kulianza kuonekana filamu za Kizungu zilizoletwa na wakoloni kwa
lengo la kuimarisha utawala wao katika koloni la Tanganyika. Katika miaka ya
1930 Tanganyika ilichaguliwa kama kituo cha kimataifa cha filamu kilichokuwa
chini ya Wamisheni ambacho kiliitwa BEKE (Bantu Educational Kinema
Experiment). Utengenezaji wa filamu katika kipindi cha ukoloni nchini
Tanzania, unaweza kuangaliwa kuanzia miaka ya 1933 hadi 1960.

Mponguliana (1982) anaeleza kuwa historia ya filamu Tanzania imegawanyika


katika vipindi viwili, yaani wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni. Vipindi hivi
vilitofautiana kulingana na matukio yaliyokuwa yakitokea wakati huo. Kwa
mfano, filamu zilizoonyesha harakati za kupigania uhuru zilitengenezwa wakati
wa ukoloni. Baada ya ukoloni, filamu zilibeba maudhui yaliyoendana na
harakati za Azimio la Arusha. Mgawanyo huu ni muhimu hasa katika utafiti huu
kwani unatusaidia kutathmini endapo filamu za sasa pia huakisi kinachotokea
katika jamii ya Kitanzania wakati huu. Pia itatusaidia kuonyesha maendeleo ya
filamu katika vipindi mbalimbali kama baada ya Azimio la Arusha na wakati wa
uchumi au soko huria.

Filamu Kipindi cha Ukoloni


Notcutt na Lathan (1937) wanaeleza kuwa katika kipindi cha ukoloni filamu
zilitumika katika mchakato wa kutawala, kuwatia kasumba na kuwapumbaza
Watanganyika. Wakoloni walianza kwa kuingiza filamu kutoka nchini
Uingereza ambazo ziliakisi mienendo na utamaduni wa kikoloni. Utengenezaji
wa filamu Tanganyika ulianza kati ya miaka ya 1935 na 1936 chini ya kampuni
iliyojulikana kama Bantu Educational Cinema Experiment. Makao yake makuu
yalikuwa Vugiri katika milima ya Usambara, Tanga, ambapo mtunzi alikuwa
Notcutt na Waingereza wenzie. Filamu nyingi zilizotengenezwa kipindi hiki
zililenga kueneza elimu ya kikoloni na kuimarisha ukoloni. Birihanze (1971)
katika Jarida la UMMA anaeleza kuwa katikati ya miaka ya 1960 TANU iliamua
kuanzisha Kampuni ya Filamu ya Taifa (TFC). Anasema kwamba hata baada ya
kuanzishwa kwa kampuni ya filamu ya taifa hakuna sera zilizowekwa kuhusiana
na filamu.

Mponguliana (1982) anaelezea kuwa filamu za mwanzo nchini Tanzania


zilitumia lugha ya Kiingereza na maneno machache ya Kiswahili, Kisukuma na
lugha nyingine za kikabila. Anaendelea kueleza kuwa utengenezaji wa filamu za
kifasihi ulianza Tanganyika miaka ya 1950. Filamu hizi zilizingatia vigezo vya
kifasihi kama vile fani, maudhui, maana, muktadha wa kifasihi, na matumizi ya
lugha yenye mvuto iliyosheheni tamathali za semi. Baadaye, kampuni ya Afrika
Kusini ilipewa jukumu la kutengeneza filamu kwa kutumia mandhari na
waigizaji wa Tanganyika na kwa lugha ya Kiswahili katika mikoa ya Dar es
salaam na Dodoma.

Filamu Baada ya Ukoloni


Kipindi hiki kinaanzia mwaka 1961, yaani baada ya Tanganyika kupata uhuru,
na kuendelea mpaka miaka ya 1990. Toka kipindi hicho kumekuwa na
mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali za maisha kama siasa,
utamaduni, hali ya uchumi, na mtindo wa maisha ya watu kwa ujumla. Hali hii
imeathiri kazi mbalimbali za fasihi kwa kuzifanya ziwe na sura mbalimbali.
Mponguliana (1982) na Mwakalinga (2003) wanaelezea kuwa katika miaka ya
1960 kulikuwa na jitihada za awali za kufufua tasnia ya filamu nchini Tanzania.
Katika kufanikisha hilo mwaka 1963 ilianzishwa Kampuni ya Filamu ya Taifa
(NFC) iliyokuwa na jukumu la kusimamia maadili katika utengenezaji wa
filamu, na shughuli nzima ya uendeshaji wa filamu nchini Tanzania.

Mwaka 1964 wataalamu wa filamu kutoka Yugoslavia walifika Tanzania


kupanga upya masuala ya filamu. NFC ilisaidia katika kutengeneza filamu za
makala simulizi zilizoelezea mambo halisi kutegemeana na matukio maalumu
kama vile ziara za kitaifa, gwaride na shughuli nyingine muhimu. Kati ya filamu
hizo ni Tanganyika Triumphant (1962), Road Ahead (1963) na The Land of
Promise (1963). Kwa sasa, filamu hizi zinatumika katika kuonyesha
kumbukumbu za matukio ya kitaifa kama vile Siku ya Uhuru. Wakati wa Azimio
la Arusha filamu ilikuwa chombo muhimu katika kutangaza sera za Ujamaa na
Kujitegemea, na Vijiji vya Ujamaa. Wakati huo TANU ilikuwa mstari wa mbele
katika kuendeleza filamu nchini Tanzania. Filamu wakati wa sera ya Siasa ya
Ujamaa na Kujitegemea zililengwa kuonyesha masuala kama vijiji vya ujamaa,
elimu ya kujitegemea na ukombozi. Kwa ufupi, filamu zilizotolewa wakati wa
Azimio la Arusha zilihamasisha harakati za ukombozi. Lakini, kwa upande
mwingine, mabepari waliokuwepo wakati ule walitumia filamu na televisheni
kama chombo cha kutekeleza matakwa ya ubepari, urasimu na propaganda.

Kulikuwa na juhudi za kuwachanganya Watanganyika kwa kuwaonyesha filamu


za Kizungu ambazo hazikuwa na uhusiano na mambo yaliyokuwa yanatokea
kwenye jamii ya Kitanganyika. Walitumia filamu kupinga itikadi ya kijamaa ili
kuwanyima au kuwanyang’anya Watanganyika ari ya kuzitazama filamu
zilizolenga kuusimika ujamaa na kuhamasisha ukombozi. Filamu nyingi
zilizoingizwa Tanganyika wakati ule zilikuwa za Kizungu na zilitengenezwa
kwa ajili ya soko la Marekani. Mfano wa filamu hizo za kibepari ni kama vile
Hammer na Slaughter. Wahusika na mandhari iliyotumika katika filamu hizi
ilikuwa ni ya Kizungu. Mathalani, katika filamu ya Slaughter, kulikuwa na
wahusika Jim Brown na ex-Green Beret ambao walikuwa askari wa kibepari wa
Marekani. Filamu hizi zilioonyesha matukio ya vurugu, ngono, matukio ya
kikatili na makosa ya jinai kama mauaji. Hii iliwafanya Watanganyika, na
Waafrika kwa ujumla kuwa na woga katika harakati za ukombozi za kupigania
haki zao Birihanze (1971:43) katika Jarida la UMMA.

Mponguliana (1982) anaeleza kuwa filamu zilizochezwa na wasanii wa


Kitanganyika zilianza kuonekana kati ya miaka ya 1960 na 1970. Filamu ya
kwanza inayojulikana kama Muhogo Mchungu ilitoka miaka hiyo na ilichezwa
na Rashid Mfaume Kawawa ambaye kwa wakati huo alikuwa miongoni mwa
viongozi wa nchi. Rashid Mfaume Kawawa, alichukua uhusika na kucheza
kama wahusika wengine. Hii ilifuatiwa na Fimbo ya Mnyonge iliyotoka mwaka
1974. Harusi ya Mariam pamoja na Yomba Yomba zilitoka mwaka 1983.
Kutazama mapitio haya ya historia ya filamu Tanzania kutasaidia kuonyesha
jinsi tasnia ya filamu ilivyopiga hatua, na kuonesha inakoelekea.

Kuanzia miaka ya 1980, kumekuwa na kushamiri kwa tasnia ya filamu kutokana


na mfumo wa soko huria. Katika kipindi cha soko huria yaani kuanzia miaka ya
1990 kulikuwa na uhuru wa kuanzisha makampuni binafsi ya habari na kazi
mbalimbali za sanaa. Mfumo wa soko huria ulichochea makampuni binafsi
kuwa na mwamko wa kufadhili filamu zilizokuwa na dhumuni la kuelimisha
watu/ jamii katika nyanja mbalimbali kama masuala ya kijamii na ya kiuchumi.
Kushamiri kwa tasnia filamu kumeendelea mpaka miaka ya karibuni yaani
miaka ya 2000 na ambapo soko la filamu limechukua sura mapya na limepiga
hatua kwa kuwa na wasanii wengi (Kabore 2003: 171).
UCHAMBUZI WA VIPENGELE VYA NAUDHUI KATIKA FILAMU ZA
TASWIRA NA VITA YA USHINDI

Dhamira katika Filamu ya Taswira


Katika filamu hii dhamira mbalimbali zimejitokeza, tunazijadili kama ifuatavyo:

Nafasi ya Elimu Katika Jamii

Elimu ni suala la msingi katika maisha ya mwanadamu, na ni kitu muhimu


katika jamii yoyote ile kwani humfanya mtu awe na uwezo wa kupambanua vitu
na kupambana na mazingira yake (Muhura 2009: 161). Kwa jumla, elimu
huwasaidia wanajamii kupata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kufanya
shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Elimu ni urithi wa taifa. Wapo waandishi
ambao wamezungumzia suala la elimu katika fasihi. Msokile (1993: 22-23)
katika uhakiki wa riwaya ya Shida ameeleza kwa kirefu suala la elimu kwa
kuwatumia wahusika Chonya na Matika. Msokile anaona kuwa elimu ni
chombo cha ukombozi na msingi mkubwa wa kumfanya mtu apate maarifa ili
aweze kupata kazi na kuwa na uwezo wa kufanya shughuli nyingine za
kimaendeleo.

Katika filamu ya Taswira suala la elimu limeonyeshwa kwa kiasi kikubwa, na


msako huu wa elimu umeweza kusukuma mbele ploti ya filamu na kuibua
matukio na dhamira mbalimbali. Filamu hii inaonyesha jinsi umaskini
unavyosababisha wanafunzi wa kike kama Trace kupata matatizo wanapotaka
kujiunga na vyuo vikuu. Kutokana na haja ya kupata elimu, umasikini, uwezo
mdogo wa kifedha walionao wasichana wengi huwashawishi kujiingiza katika
njia za mkato za kutafuta pesa ambazo aghalabu si halali, kama kuuza miili yao
ili waweze kupata pesa. Kwa mfano, wapo wasichana wa vyuo vikuu hapa
nchini ambao hujihusisha na masuala ya kuuza miili yao ili wapate fedha za
kutumia vyuoni. Hali hii inaonyesha jinsi wanafunzi wasichana yanavyoweza
kukumbana na matatizo mbalimbali katika harakati za kutafuta elimu.

Athari za Ubinafsi
Ubinafsi ni hali au tabia ya mtu au watu wachache kufanya vitendo au vitu
fulani ili kuweza kujinufaisha wao wenyewe bila kujali maisha ya wengine
(Muhura 2009: 81). Katika filamu ya Taswira, ubinafsi unajitokeza kwa
kumuangalia mhusika James ambaye anataka kutumia mali ya urithi kwa
manufaa yake binafsi bila kumshirikisha ndugu yake, Tamala. James anatumia
mali hii na mke wake Jesca, ambapo baadaye anapata fundisho kwa mkewe
Jesca kumkimbia baada ya kumfilisi. Pia ubinafsi unajitokeza kwa kumuangalia
mhusika Dkt Gumbo ambaye alijali maisha yake na ya familia yake tu, bila
kuwajalia wengine, yaani, Tamala na Trace ambao aliwapa ujauzito na
kuwatelekeza. Katika filamu hii ubinafsi unasababisha wahusika wengi
kutelekezwa, kuhangaika kwa mateso na hatimaye wengine kufa. Matokeo ya
ubinafsi wa James na Dkt. Gumbo yanasababisha maisha ya Tamala yawe ya
kuhangaika na kutangatanga, kwani mwishowe Tamala anarudi kijijini na kuishi
maisha ya taabu huku kaka yake (James) akitumia mali ya urithi pamoja na
Jesca, mkewe. Pia ubinafsi wa Dkt Gumbo ulisababisha Trace kufariki dunia.

Umalaya na Ngono Zembe


Umalaya na ngono zembe ni hali ya mtu kuwa na wapenzi wengi na aghalabu
kufanya kitendo cha ngono bila kutumia kinga. Zipo kazi mbalimbali za fasihi
ambazo zimezungumzia suala la umalaya na ngono zembe. Kwa mfano,
Mponda (1988) amejadili suala la umalaya kwa kuangalia riwaya ya Nyota ya
Huzuni. Katika riwaya hii Makokoto amesawiriwa kuwa na tabia ya umalaya.
Huyu ni mwanaume wa makamo ambaye ni mzinzi na mlevi. Kutokana na
uzinzi wake amesababisha madhara makubwa kwa watu wa jamii yake.

Katika filamu ya Taswira masuala ya umalaya na ngono zembe ni dhamira


ambazo zimejitokeza kwa kiasi kikubwa. Umalaya unajidhihirisha kwa
kumuangalia Dkt. Gumbo alivyokuwa akijihusisha na mapenzi holela na
wanawake tofautitofauti kwa nyakati tofauti, kama vile Tamala, Trace na Mama
Sospeter, mkewe, bila kutumia kinga. Kutokana na tabia yake hiyo, Dkt. Gumbo
alimsababishia Tamala ujauzito na kumtelekeza. Pia anajikuta akijihusisha
katika mapenzi na binti yake Trace, bila kujua kwamba ni binti yake aliyezaliwa
na Tamala baada ya yeye kumtia ujauzito Tamala na kumtelekeza. Hii
inajidhihirisha pale Dkt. Gumbo anaposema, “Hivi wewe hujui kuwa mimi nina
mke wangu? Je, mke wangu akijua unadhani itakuwaje?” Maneno haya
aliyasema kwa Tamala na Trace kwa nyakati tofauti. Hii hii inaonyesha kuwa
Dkt. Gumbo alitaka kufanya nao mapenzi kutimiza haja zake za kimwili na
hakuwa na mapenzi ya dhati kwao.

Katika jamii ya Kitanzania, suala la umalaya na ngono zembe linatokea kwa


vijana na hata watu wazima. Kwa upande wa wasichana, masuala ya umalaya na
ngono zembe yamesababisha matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata
mimba zisizotarajiwa. Pia, umalaya umehatarisha afya za watu, wanawake kwa
wanaume kwa kuwaweka katika uwezekano wa kupata maambukizi ya
UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa. Wapo wasichana ambao wamebakwa
na wengine wamelazimika kukubali ngono zembe kutokana na shida
mbalimbali za kimaisha. Pia, ukosefu wa huduma muhimu kutoka kwenye
familia zao na ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya athari ya ngono zembe
kumewafanya wasichana kujiingiza katika kufanya ngono zembe. Hivyo basi, ni
jukumu la Watanzania kupiga vita umalaya na ngono zembe kwa kuwa
waaminifu katika mapenzi.

Ndoa na Uhusiano wa Kimapenzi


Wapo wasanii mbalimbali ambao wamezungumzia suala la ndoa na uhusiano wa
kimapenzi. Zipo nyimbo, mashairi tamthiliya na kazi nyingine za kifasihi
ambazo zimeangalia suala hili. Kwa mfano, baadhi ya mashairi ya Shaaban
Robert yanaonyesha suala la ndoa na uhusiano wa kimapenzi. Katika kitabu cha
Mapenzi Bora (1970), Shaban Robert anazungumzia kwa kirefu suala la
mapenzi kuwa ni mwangaza na taa katika giza, na kuwa mapenzi yana baraka
na huondoa ubaguzi baina ya watu. Kwa mujibu wa Muyaka kama
alivyonukuliwa na Senkoro ( 2007: 151- 152), amezungumzia masuala
mbalimbali kama vile mapenzi. Kwa mfano, katika shairi la “Mahaba” anaeleza
jinsi mapenzi yalivyo na nguvu, kwani yanapomuingia mtu huwa kama
mpumbavu, wala hasikii na haoni ubaya wowote kwa muhibu wake. Mtu akiwa
na hali hii hajali yasemwayo. Mapenzi ya kweli huleta raha ndani ya roho. Kwa
hiyo hapa mapenzi yamezungumzwa kwa upande chanya. Katika filamu ya
Taswira, suala la uhusiano wa kimapenzi limezungumziwa kwa kirefu. Matukio
na matendo ya wahusika yanatawaliwa na uhusiano wa kimapenzi. Hii
inajidhihirisha kwa kumuangalia Dkt. Gumbo ambaye alikuwa na uhusiano wa
kimapenzi na mkewe, Mama Sospeter, Tamala na Trace. Mapenzi haya
yanaonekana kuwa hayakuwa ya kweli kwani Dkt. Gumbo hakuwa mwaminifu
kwa mkewe, na aliwakana na kuwatelekeza Tamala na Trace hasa pale
walipompa taarifa kuwa ni wajawazito. Dkt. Gumbo alionekana kushangazwa
na kuamua kukana ujauzito na kuwalazimisha watoe mimba hizo. Hii
inaonyesha jinsi Dkt. Gumbo alivyokuwa hana mapenzi ya kweli ila tu alitaka
kutimiza shida na haja zake za kimwili. Angelikuwa na mapenzi ya kweli
angelikubali ujauzito na kuahidi kuwatunza watoto.
Uhusiano mwingine wa kimapenzi unajionyesha kati ya Sospeter na Trace.
Sospeter ana mapenzi ya kweli kwa Trace ila anabadili nia yake baada ya kuona
kuwa Trace anataka kumsingizia ujauzito ambao si wake. Kwa mantiki hiyo,
inaonekana kwamba mapenzi ya kweli yanahitaji uaminifu. Katika jamii ya
Kitanzania kumekuwa na migogoro na usaliti katika uhusiano wa kimapezi
kutokana na kukosa uaminifu na utu baina ya watu. Watu wanafarakana kwa
sababu ya kukosa uaminifu. Ili kuwepo na mapenzi ya kweli inabidi kufuata
maneno kama ya Shaaban Robert katika kitabu chake cha Mapenzi Bora
(1975:26) ubeti wa 360 ambapo anaelezea kuwa mapenzi huchukuliwa kama
upendo wa kweli na urafiki na yanayofanya moyo usisikitike, yanayojali usawa
na haki na huzuia majonzi. Hii inamanisha kuwa mbali na uaminifu lazima
kuwepo na upendo na urafiki, usawa na haki ndipo mapenzi yatakuwa ya furaha
na yenye kudumu.

Usaliti
Usaliti, ambao waweza kuhusisha utapeli na udanganyifu, ni dhamira ambayo
hutawala katika kazi mbalimbali za fasihi kama vile tamthilia, riwaya, hadithi
fupi na filamu. Katika filamu ya Taswira, dhamira hii inajidhihirisha kwa
kuwaangalia Jesca, Dkt. Gumbo, James na Trace. Jesca hakuwa na mapenzi ya
kweli kwa James. Nia yake ilikuwa kumfilisi, kwa kuuza mali zote na
kukimbilia Botswana na wanae, akimwacha James hana kitu. Kwa upande
mwingine, Dkt. Gumbo anamsaliti mkewe kwa kuwa na uhusiano wa
kimapenzi nje ya ndoa. Lakini hata nje pia anaishia kuwatelekeza anaowapa
ujauzito. Kwa mfano, anamtelekeza Tamala baada ya kumpa ujauzito. Vile vile
Dkt. Gumbo anamlaghai Trace kwamba atamsomesha na hatimaye anambaka na
kumtelekeza baada ya kumpa ujauzito.
Udanganyifu unaendelea kujitokeza pale ambapo Trace anamua kujihusisha
katika mapenzi na Sospeter ili aweze kumsingizia ujauzito aliopewa na Dkt.
Gumbo. Tatizo au hali kama hii ya kusingizia ujauzito inajitokeza katika jamii
ya Kitanzania. Wapo wanawake na wasichana ambao wanapewa ujauzito na
kujaribu kuwasingizia watu wengine ili waweze kupata matunzo. Hii hutokana
na kutelekezwa na anayehusika na ujauzito huo. Pia hali ngumu ya maisha
huwafanya wanawake na wasichana hao kufanya udanganyifu kama huo.
Madhara ya usaliti na udanganyifu katika ndoa au uhusiano kwa ujumla
yanaweza kufarakanisha familia kwa kuleta migogoro isiyokwisha na kurudisha
maendeleo nyuma kutokana na kukosa umoja kati ya watu. Kwa jumla, usaliti,
utapeli na udanganyifu katika uhusiano wa kimapenzi hutokea kwa kiwango
kikubwa katika jamii ya Kitanzania. Wapo wasichana wadogo na wanawake
ambao wamekumbwa na kuathirika na hali kama hii, na, imewasababishia
kukata tamaa na hatimaye kujiua wanapoona kuwa hawana pa kukimbilia. Hali
hii inawapata hasa wanawake wa umri mdogo ambao hawawezi kusimama peke
yao, na kwa kiasi fulani inatokea kwa watu wazima pia.

Ubakaji
Kubaka ni kitendo cha kufanya tendo la ngono na mtu bila ridhaa yake. Idadi ya
matukio ya ubakaji inayozidi kuongezeka kuripotiwa kwenye vyombo vya
habari inadhihirisha jinsi ubakaji ulivyo tatizo kubwa katika jamii ya Kitanzania.
Matukio hayo yanahusisha watu wazima wanaobaka watoto wadogo, vijana
wanaobaka vijana wenzao, watu wazima kubaka watu wazima wenzao, na
wanaume (na vijana) wanaobaka vikongwe. Katika filamu ya Taswira ubakaji
unajitokeza pale Dkt. Gumbo anapombaka Trace, na hatimaye, kumpa ujauzito
na kumtelekeza. Matukio ya ubakaji hutokea sehemu nyingi kama sehemu za
kazi na waathirika wengi ni wanawake, ambao huishia kupata mimba na
maradhi. Aidha, wanaume wabakaji hujiongezea nafasi za kupata maambukizi
ya magonjwa ya zinaa. Matatizo haya ya kubakwa, hutokea wakati wa kutafuta
nafasi za ajira, nafasi za masomo au misaada mbalimbali. Pia, upo ubakaji wa
vikongwe na watoto wadogo, ambao, huweza kufanyika kwa ajili ya imani za
kishirikina.

Athari za Tamaduni za Kigeni

Suala la athari za tamaduni za kigeni hasa kwa vijana limezungumziwa na


wataalamu mbalimbali wa fasihi. Dhamira hii pia inajitokeza katika umbo la
mgongano wa tamaduni kati ya utamaduni wa jadi wa Kiafrika na utamaduni wa
Kimagharibi. Suala hili limejadiliwa katika tamthiliya za Ibrahimu Husein
(Wakati Ukuta na Kwenye Ukingo wa Thim), Penina Muhando (Hatia), Ngugi
wa Thiongo (Nimerogwa Nisiwe na Mpenzi), na Euphrase Kezilahabi katika
riwaya zake tatu za Kichwa Maji, Dunia Uwanja wa Fujo, na Rosa Mistika.
Wote hawa kwa viwango tofauti wameonyesha jinsi vijana au kizazi kipya
kilivyoathiriwa na tamaduni za kigeni mpaka kufikia mahali ambapo vijana
hawajui waegemee upande gani.

Katika jamii ya Kitanzania upo uzoefu na taratibu za maisha ambazo


zimezoeleka na zinategemewa zifuatwe na wanajamii. Taratibu hizi za maisha
zaweza kuwa mila na desturi, mavazi, kusalimiana na uhusiano katika jamii.
Kutokana na mwingiliano wa tamaduni mbalimbali kutoka nchi za kigeni
taratibu hizi za maisha zimebadilika, na watu wanadai kwamba wanakwenda na
wakati. Ngugi wa Thiong’o (1968) katika tamthiliya ya The Black Hermit, na
p’Okot Bitek katika Wimbo wa Lawino (1975) wanakubaliana kwamba ukoloni
na Ukristo ndizo sababu kuu zilizozusha mgogoro baina ya imani ya Mwafrika
na ile ya Mzungu. Waandishi hawa wanasisitiza kuwa maisha ya Mwafrika
yalivurugwa na Mzungu. Uvurugaji huu uliwafanya baadhi ya watu weusi
kukosa mizizi kabisa, wakawa wanayumbayumba baina ya tamaduni
wasizozifahamu vizuri.

Mathalani, katika tamthiliya ya Wakati Ukuta, mwandishi ameonyesha jamii


ambayo imevamiwa na utamaduni wa kigeni, au usasa. Mara nyingi vijana huwa
wa kwanza kufuata mienendo na matendo mapya ya maisha kwa kuwa huwa
hawajazama katika mfumo maalumu wa maisha na wana tamaa zaidi ya
kujaribu mienendo mipya. Kwa hiyo, ni rahisi kwa vijana kubadilika kwa vile
imani zao za kimsingi huwa zinaendelea kujengeka (Wafula 1999: 18). Katika
uigaji huu wa tamaduni za kigeni kumepelekea kuwa na mmomonyoko wa
maadili ambao umewafanya watu au wanajamii fulani kuenenda kinyume na
mazoea, mila na desturi zao na utamaduni wa jamii kwa ujumla. Mila na desturi
hizo huweza kuwa mavazi yaani jinsi watu wanavyovaa, mtindo wa maisha na
uhusiano na mienendo ya watu kwa ujumla (Chiraka 2009:14).

Katika filamu ya Taswira kuna viashirii vinavyoonyesha athari za tamaduni za


kigeni ambazo zimesababisha mmomonyoko wa maadili. Hii inajidhihirisha
kwa kuangalia tabia za wahusika mbalimbali ambao wanaenda kinyume na
maadili, mila na desturi za jamii ya Kitanzania. Kwa mfano, mtindo wa maisha
na mahusiano ya watu katika familia ya akina Sospeter ni mtindo wa ambao
umeegemea zaidi Magharibi. Kwa mfano, tabia ya kukumbatiana na kubusiana
hadharani, hasa baina ya watoto na wazazi wao, ni kiashirii cha athari za
utamaduni wa kigeni. Uhusiano wao katika familia hauoneshi uzoefu wa maisha
ya Kitanzania na ya Kiafrika kwa jumla.
Pia mtindo wa uvaaji wa Trace unaashiria kuathiriwa na tamaduni za kigeni. Hii
inawakilisha uvaaji wa wasichana wengi hasa waishio mijini ambao wameiga
uvaaji wa Kimagharibi. Mitindo hiyo ya uvaaji inahusisha mitindo ya nywele ya
kigeni, kuvaa nguo fupi (sketi fupi), uvaaji wa blauzi ambazo zinaonyesha
sehemu kubwa ya matiti na ambazo huweza kusababisha vishawishi vya
kingono kwa wanaume. Kwa mtazamo wa mtafiti, uvaaji wake huo ndio
ulimfanya hata Dkt. Gumbo amtamani Trace kimapenzi, kwani alikuwa akivaa
sketi fupi zinazoonyesha maumbile na pia blauzi ambazo zilionyesha sehemu
fulani ya matiti yake. Hii inaashiria kuathiriwa na tamaduni za kigeni.

Vile vile, zipo kazi nyingine ambazo zinaonyesha athari za uigaji wa tamaduni
za kigeni. Kwa mfano, katika Wimbo wa Lawino uliotungwa na p’ Okot Bitek
(1975), Lawino ambaye alikuwa akidumisha mila na desturi za Kiafrika
anaonekana kumkosoa Clementine ambaye ameathiriwa na tamaduni za kigeni
kwa kuiga mtindo wa mavazi na nywele na hata kupaka rangi ya mdomo pamoja
na uvaaji kwa ujumla, (u.k. 39). Mwandishi anaonyesha jinsi Clementine,
mwanamke wa kisasa, anavyoiga utamaduni wa Kimagharibi ambapo
anawakilisha wanawake wengi ambao wanaiga mitindo ya uvaaji bila kujali
mila na desturi zao.

Pia matumizi ya maneno ya Kiingereza wakati wa kuongea Kiswahili, yaani


uchanganyaji misimbo ni kiashirii kimojawapo cha kuonyesha athari za
utamaduni wa kigeni. Kwa mfano, wahusika Sospeter na Trace wanaonekana
wakitumia maneno machache ya Kiingereza katika maongezi yao, hasa pale
Sospeter anapomwambia Trace, “Let’s just be friends” (ikimaanisha kuwa
naomba tuwe marafiki tu). Sospeter alimwambia Trace maneno hayo alipoanza
kumtamani kimapenzi. Matumizi ya majina ya Kizungu pia yanaweza kuwa
kiashirii cha athari za utamaduni wa kigeni. Majina hayo ni kama: Trace,
Sospeter, James na Jesca. Majina ambayo yangefaa kutumika kama kiashirii cha
Utanzania ni yale yenye asili ya Kibantu kama Baraka, Bwana Maige, Majuto
ambayo hutolewa kimila bila kubatizwa. Waandishi wengi wa Kiafrika hasa
Ngugi wa Thiong’o, Chinua Achebe na p’Okot Bitek wanaonyesha katika kazi
zao jinsi walivyokuwa wakipinga tamaduni za kigeni ambazo zililetwa na
wakoloni ukiwemo Ukristo, majina ya Kikristo na utamaduni wa Kimagharibi
kwa ujumla.

Katika jamii ya Kitanzania athari za tamaduni za kigeni zinajidhihirisha pia kwa


vijana wengi kuathiriwa na mtindo wa uvaaji wa Kimagharibi. Kwa mfano,
akina dada kuvaa nguo fupi yaani (vimini) kwa lugha ya mtaani, ni kudhihirisha
kuwa wanakwenda na wakati. Matokeo yake tunaona kuwa kesi za kubakwa
zimekuwa nyingi. Athari nyingine ni kwamba, wakipita mitaani
wanadhalilishwa kijinsia kwa kutukanwa na kutaniwa na vijana au watu wa
jinsia ya kiume. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani uvaaji huo usivyokubalika
katika jamii yetu ya Kitanzania.

Jamii ya Kitanzania inawatarajia wanawake au akina dada kuvaa nguo ndefu ili
kujisitiri, lakini kutokana na utandawazi watu wanaiga utamaduni wa kigeni bila
kuangalia mazingira na madhara yake. Kwa ujumla athari za tamaduni za kigeni
zimeanza toka wakoloni walipoingia nchini Tanzania, tokea utawala wa Wareno,
Wajerumani na Waingereza. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, hali hii
imezidi kuongezeka kutokana na utandawazi na kukua kwa teknolojia ya
vyombo vya habari na mfumo wa kijigitali. Kwa jumla, hali hii imeathiri sana
utamaduni wa Mtanzania kiasi kwamba tunashindwa kutofautisha utamaduni wa
Mtanzania ni upi na wa kigeni ni upi. Utamaduni wa Mtanzania umepoteza dira
kutokana na mwingiliano wa tamaduni. Athari hizi za tamaduni za kigeni
zimechangiwa na mataifa yanayoendelea kuiga mambo yanayoendelea katika
mataifa yaliyoendelea. Hii inajitokeza kwa kuangalia suala la utandawazi
ambapo mataifa yanayoendelea hulazimika kuiga mambo ambayo yako nje ya
utamaduni.

Katika kudhibiti uigaji wa tamaduni ambazo zinakiuka maadili na utamaduni wa


Kitanzania, ipo bodi ya filamu ambayo inasimamia mambo hayo. Kwa kuwa
filamu zinatakiwa kudumisha utamaduni na maadili ya jamii, ziko filamu
ambazo zilifungiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kutokana na kukiuka taratibu
za kimaadili. Filamu hizo zilihusika na kuonyesha masuala ya uhusiano wa
jinsia moja. Baadhi ya filamu ambazo zimeonekana kumomonyoa maadili ni
pamoja na Mtoto wa Mama. Inye Plus, Inye Ndembendembe na Inye
Gwedegwede ambazo zinalaumiwa kwa kuharibu utamaduni na maadili ya
Kitanzania kwa kuonesha mavazi na matendo yasiyokubalika katika jamii.
Filamu hizo zimeondolewa katika soko kwa sababu pamoja na mapungufu
mengine, zinachochea uhusiano wa jinsia moja

( Daily News ya tarehe 28 Aprili 2011).

Malezi bora, Adabu na Utu

Suala la malezi na utu bora limezungumziwa na baadhi ya waandishi katika kazi


zao. Taib (2009: 137-138) anamwelezea mwandishi Shaaban Robert katika kazi
zake kuwa anaongozwa na falsafa ya utu katika maisha ya mwanadamu.
Maelezo haya yanapatikana katika kitabu cha Maisha Yangu Baada ya Miaka
Hamsini (uk.100). Mwandishi anaendelea kusema kuwa utu unaonekana pia
katika kazi zake mbalimbali kama Utu Bora na pia katika shairi la “Adabu” ( u.k
4). Malezi bora na adabu ni mambo ambayo yanajenga utu wa mwanadamu,
kwani humaanisha kuwa mtu mwenye adabu ndiye mwenye utu. Kwa mtazamo
wa Shaaban Robert, suala la malezi bora, adabu, heshima, hekima na utu ni vitu
ambavyo vinaendana na vina uhusiano wa karibu.

Katika filamu ya Taswira, dhamira iliyotajwa hapo juu imejitokeza kwa


kuangalia matendo ya mhusika Sospeter ambaye alilelewa katika malezi bora na
akawa mtu mwenye adabu, heshima, hekima na utu katika kuwasaidia wengine.
Hii inajidhihirisha pale ambapo Sospeter anaonyesha heshima kwa wazazi wake
na pia kwa Tamala. Sospeter anakubali kuishi na Trace nyumbani kwao na
kuonyesha upendo na kumjali. Hekima inajionyesha pale ambapo Sospeter
anaamua kuwapatanisha na kuwaunganisha baba yake na Tamala, hususani pale
anaposhauri wamchukue mama Trace (Tamala) kutoka kijijini ili aende kuishi
nao mjini. Hii inatokkea baada ya Mama Sospeter na Trace kufariki. Baada ya
kuafikiana na baba yake, Sospeter anamfuata Tamala kijijini.

Katika jamii ya Kitanzania suala la malezi bora, utu, wema, heshima, hekima
yanatokea katika jamii yetu. Wapo wazazi ambao wanawalea watoto wao katika
malezi mazuri ambayo yanawafanya watoto hao kuwa na heshima na upendo
wa kujali wengine wenye shida. Kwa upande mwingine, wapo wazazi ambao
hawawalei watoto wao katika maadili na kuwasababishia kukosa upendo, moyo
wa kujali wengine na hatimaye kukosa heshima na hekima, kwani mtoto
umleavyo ndivyo akuavyo.

Mimba Nje ya Ndoa na Athari za Utoaji Mimba

Mimba nje ndoa na utoaji mimba ni masuala ambayo yanawakumba wasichana


wengi katika jamii ya Kitanzania. MOEVT (2006) inaeleza kuwa mimba nje ya
ndoa huwapata wasichana katika umri mdogo kutokana sababu mbalimbali.
Sababu hizo ni kama vile mila na desturi za jamii ambazo huweza kuwachochea
kufanya mapenzi katika umri mdogo. Sababu za kiuchumi kama hali ngumu za
maisha huweza kuwafanya wasichana kujihusisha na masuala ya kimapenzi
wakiwa katika umri mdogo sana. Pia sababu nyingine ni tabia tu za wasichana
kupenda kujihusisha na masuala ya ngono katika umri mdogo na hii
husababishwa na mabadiliko ya kibaiolojia yanayotokea kwenye miili yao
ambayo huwafanya wasichana kuwa na tamaa au mihemko ya kufanya mapenzi
bila kuchukua tahadhari.

Katika filamu ya Taswira, hali hii inajidhihirisha pale ambapo Dkt. Gumbo
anafanya mapenzi na Tamala na kumsababishia ujauzito, hatimaye kumtelekeza
bila kufuatilia taarifa zozote za mama na mtoto. Hii inasababisha afanye
mapenzi na Trace na kumpa ujauzito bila kujua kwamba ni binti yake. Baadaye
Dkt. Gumbo anamwambia Trace atoe mimba hiyo kwa kuwa eti ingeleta
mgogoro katika ndoa yake. Trace hakubaliani na uamuzi wa Dkt. Gumbo kwa
sababu anajua athari za utoaji mimba. Hii inaonyesha kuwa alikuwa na elimu ya
kutosha kuhusiana na athari za utoaji mimba na anamwambia Dkt. Gumbo kuwa
amtafutie nyumba yake ya kuishi. Baada ya mke wa Dkt. Gumbo kupata taarifa
za ujauzito wa Trace anamlaghai Trace kwa kumpa dawa ambazo anadai kuwa
zingemsaidia katika ukuaji wa mimba. Badala yake dawa hizo ni za kutoa
mimba, na, zinamfanya Trace kupata maumivu makali na baadaye kupelekwa
hospitali na kufanyiwa upasuaji. Katika tukio hilo, madaktari wanafanikiwa
kumuokoa mtoto lakini, kwa bahati mbaya, Trace anapoteza maisha. Kifo cha
Trace kinaonyesha jinsi mabinti wanavyoweza kuhatarisha maisha yao kwa
kujaribu kunywa madawa ya kutoa mimba. Pia, inaonyesha jinsi wasichana
wanavyopata matatizo katika kulea mimba hizo kama vile kukosa matunzo,
kutelekezwa na hatimaye vifo.
Katika jamii ya Kitanzania suala la mimba nje ya ndoa na utoaji mimba
linatokea sana hasa kwa wasichana wa umri mdogo. Kama ilivyolezwa hapo
awali kuwa zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. Wasichana na
wanawake walioathirika na tatizo hilo wamefikia hata kuwatupa watoto
majalalani kutokana na ugumu wa maisha na kutokuwa tayari kubeba mimba
hizo na kutunza watoto. Hii inatokana na kukosa elimu ya kutosha juu ya
kujikinga na mimba nje ya ndoa. Kuhusiana na suala la utoaji mimba, kwa
mfano, wapo madaktari ambao badala ya kuwaelimisha wanawake juu ya athari
za utoaji mimba wao wanakuwa mstari wa mbele kuwashinikiza watoe mimba,
ili madaktari hao, waweze kujipatia kipato kwani utoaji mimba umekuwa kama
mradi kwa baadhi ya madaktari. Hii inaonyesha ukosefu wa maadili kwa baadhi
ya madaktari. Kwa upande wa Tanzania, suala la utoaji mimba siyo halali kwa
mujibu wa sheria. Kutoa mimba ni kosa la jinai ambalo linachukuliwa kama
uuaji. Ipo mijadala mbalimbali iliyofanyika kuhusiana na suala hili, ikiwemo
mijadala ya bungeni. Hii ni katika harakati za kupiga vita utoaji mimba, kwamba
ni kitendo kisichokubalika katika jamii ya Kitanzania. Pia ni kinyume cha haki
za binadamu.

Masuala ya Kijinsia
Dhamira hii imezungumzia nafasi ya mwanamke na mwanaume katika jamii.
Masuala ya kijinsia yanazungumziwa sana katika jamii yetu ya Kitanzania.
Kuhusiana na nafasi ya mwanamke katika jamii, wapo waandishi mbalimbali
ambao wamezungumzia suala la nafasi ya mwanamke katika jamii. Mwanamke
amesawiriwa katika nafasi mbalimbali kutegemeana na mtazamo wa mwandishi.

Katika filamu ya Taswira mwanamke amesawiriwa katika pande mbili yaani


upande chanya na hasi. Kwa upande chanya mwanamke amesawiriwa kama mtu
shupavu, asiyekata tamaa kwa haraka na jasiri wa kuweza kupambana na
vikwazo mbalimbali katika maisha. Ujasiri, ushupavu na kutokata tamaa
kunajidhihirisha kwa kuwaangalia wahusika Tamala na Trace mwenyewe.
Tamala kwa mfano, amekuwa ni mwanamke shupavu na jasiri katika
kupambana na changamoto mbalimbali zilizomkabili katika maisha. Mbali na
kutelekezwa na Dkt. Gumbo wakati wa ujauzito, anajitahidi kutunza na kulea
mimba yake mpaka anapojifungua. Mbali na hayo, Tamala anajitahidi kufanya
shughuli za kiuchumi, yaani, kilimo, ili aweze kujikwamua na hali ya maisha
aliyokuwa nayo. Mapato haya yanamsaidia katika kutatua matatizo yake kama
kulipa ada ya Trace mpaka anapomaliza shule. Anamsisitiza mwanaye pia kuwa
shupavu kwa kusema kuwa mwanamke shupavu kila mara hutafuta njia mbadala
ya kuweza kujikwamua katika maisha.” Maneno haya yanaonyesha jinsi Tamala
anavyomshauri mwanawe na kumfundisha kuwa shupavu. Trace naye
amesawiriwa kama mwanamke jasiri, shupavu na asiyekata tamaa haraka. Haya
yanajidhihirisha pale Trace anapotaka kutimiza ndoto zake za kupata elimu ya
juu. Ili kufika lengo hili, anatafuta ufadhili kwa mshauri wa wanafunzi na
anataka kujitolea figo yake ili apate fedha ya karo. Ndoto zake hazikutimia
kwani alibakwa na kupata mimba ya Dkt. Gumbo na hatimaye kufa.

Vilevile Mke wa Dkt. Gumbo amesawiriwa katika nafasi chanya kwa kuonesha
uwajibikaji wake. Amesawiriwa kama mwanamke anayefanya kazi kwa bidii
kwa kujishughulisha na biashara ya kuendesha kampuni iliyoitwa Kilua
Investment. Mama Sospeter anadiriki kwenda hata, nchi za mbali kutafuta
mawasiliano na malighafi kwa ajili ya kuendeleza kampuni, akiongozana na
mwanae Sospeter. Hii inaonyesha kuwa wanawake wanaweza kufanya shughuli
ambazo wanaume wanafanya.
Kwa upande wa pili, mwanamke katika filamu ya Taswira amesawiriwa katika
nafasi hasi kwa kumwangalia Tamala na Trace. Tamala anatumiwa kama
chombo cha starehe na Dkt. Gumbo kwa kukubaliana kufanya urafiki na,
hatimaye, kuwa na uhusiano ya kimapenzi nje ya ndoa. Katika filamu hii
mwanamke anaonekana kama chombo cha starehe pale Tamala anapopata
ujauzito wa Dkt. Gumbo na kutelekezwa. Vilevile Dkt. Gumbo anajikuta akiwa
na uhusiano kimapenzi na Trace bila kujua kuwa ni binti yake na ambaye pia
Dkt. Gumbo alimkana baada ya kupata ujauzito. Pia nafasi hasi inajidhihirisha
kwa kumuangalia Mke wa Dkt Gumbo, ambaye anaonyesha na roho mbaya na
ya kinyama ya kumdhuru Trace, pale anapompa dawa za hatari za kutoa mimba.

Katika jamii ya Kitanzania wanawake wanachukuliwa katika nafasi mbalimbali.


Wapo wanawake wanaotaka kujikomboa kutokana na matatizo mbalimbali kwa
kujikwamua wao wenyewe. Hawa wanawakilisha ukombozi wa mwanamke
ingawa wanakabiliwa na changamoto ili kufikia malengo yao. Wanawake katika
kundi la pili wanataka kupata huduma muhimu kwa kuuza miili yao lakini
mwisho wake wanaishia kupata ujauzito na maradhi. Pia kundi lingine la
wanawake ni lile la wenye roho za kinyama, ambalo linadhamiria kudhuru na
kuumiza wanawake wengine. Kwa hakika, wanawake wanapaswa kuenenda
katika njia inayofaa, inayopaswa na kuweza kuigwa na watu wengine katika
jamii. Hivyo basi, wasijidhalilishe kwa kujiona kuwa wao ni viumbe duni bali
wajitahidi kujikomboa kwa kujikwamua kwa kufanya shughuli za kiuchumi na
kuepuka utegemezi. Kwa mfano, wapo wanawake wengi wanaishi maisha kama
ya Tamala kwa kuuza vyakula, wengine wanafanya shughuli za kilimo na
biashara nyingine ndogondogo ili waweze kujikwamua katika matatizo ya
kiuchumi. Fedha wanazozipata wanazitumia katika kulipia ada za watoto wao na
kuongeza pato la familia. Tabia za akina baba wengi kutelekeza familia zao kwa
sababu mbalimbali, huwasababishia akina mama, kuwa na mzigo mkubwa wa
kulea familia. Pia wapo wasichana ambao wanaishi maisha kama ya Trace na
wanatamani maisha ya juu ambayo hawana uwezo nayo. Hii huwafanya
wasichana wengi kujiingiza katika matatizo mbalimbali. Jamii ya Kitanzania
hususani wanawake, wanapaswa kuwa makini katika kutafuta mbinu faafu za
kujikwamua kiuchumi na katika matatizo mengine pia.

Hatuwezi kuongelea masuala ya jinsia bila kugusia nafasi ya mwanaume katika


jamii. Katika filamu ya Taswira, mwanaume amesawiriwa katika nafasi mbili,
yaani nafasi chanya na nafasi hasi. Kwa upande wa nafasi chanya, Dkt. Gumbo
amesawiriwa kuwa ni baba mwajibikaji na ambaye anajali familia yake.
Anaonekana akimjali mke wake, pamoja na mwanae (Sospeter). Pili, Dkt.
Gumbo anaonekana kuwa mshauri mzuri, hasa pale anapomshauri Trace kuhusu
na hatari za kutoa figo. Kwa upande wa nafasi chanya pia, tunaweza
kumwangalia Sospeter ambaye alikuwa mwenye mapenzi ya kweli kwa Trace.
Yeye hakuwa mdanganyifu, bali Trace mwenyewe ndiye aliyekosa uaminifu.
Pia, alikuwa ni kijana mwenye busara na mshauri mzuri na mwenye utu kwa
sababu alijali shida za watu wengine, mfano familia ya akina Trace.

Mwanaume katika filamu hii ya Taswira pia amesawiriwa katika nafasi hasi,
hasa kwa kumuangalia mhusika Dkt. Gumbo kwa anaonyesha tabia ya umalaya
ya kujihusisha na mapenzi na wanawake zaidi ya mmoja huku akijua kuwa ana
mke wake ndoa. Hii inajidhihirisha kwa kumuangalia Tamala na Trace ambao
walijihusisha kimapenzi na Dkt. Gumbo mwisho wake walitelekezwa. Pia Dkt.
Gumbo amesawiriwa kuwa mnyanyasaji kwa kumnyanyasa Trace kijinsia, pale
anapombaka. Katika jamii ya Kitanzania wapo wanaume ambao wanafanya
mambo yenye manufaa kwao binafsi na kwa jamii nzima na pia wapo wale
wanaofanya mambo ambayo hayakubaliki kijamii. Wapo wanaume ambao
kutokana na hulka na mienendo yao wamekuwa wakifanya mambo ya ajabu
kama umalaya na kuwasababishia watu wengine matatizo. Wapo wanaume watu
wazima ambao wanajihusisha kufanya mapenzi na wasichana wadogo bila
kuona aibu wakidai kwamba wanakwenda na wakati.

Suala la unyanyasaji wa kijinsia na ukatili linajitokeza pia katika filamu ya


Taswira. Tunavyojua kuwa kuna aina mbalimbali za unyanyasaji wa kijinsia
kama unyanyasaji wa kimwili, kisaikolojia na kingono. Katika filamu hii ya
Taswira, unyanyasaji wa kijinsia unaojitokeza kwa kiasi kikubwa ni ule wa
kingono na ule wa kisaikolojia. Hii inajidhihirisha kwa kumuangalia mhusika
Trace ambaye ananyanyaswa kingono na kisaikolojia. Kitendo hiki cha
unyanyasaji kinafanywa na Dkt. Gumbo ambaye alimlazimisha Trace
kujihusisha kimapenzi bila ridhaa yake na kumtishia kumnyima mahitaji
ambayo alikuwa akiyategemea kutoka kwake yaani ufadhili wa kujiunga na
chuo kikuu. Kwa hiyo, Trace analazimika kujihusisha kimapenzi na Dkt. Gumbo
ili aweze kupata ufadhili.

Ukatili
Ukatili ni hali ya kumtendea mtu mwingine kitendo kisichostahili kufanywa kwa
binadamu yeyote yule. Suala la ukatili katika filamu hii linajitokeza pale
ambapo mke wa Dkt. Gumbo alipojaribu kumpa Trace vidonge vya kutoa
mimba. Mke wa Dkt. Gumbo alifanya hivyo, baada ya kugundua kwamba mume
wake ndiye aliyehusika na ujauzito huo, ambao ulisababisha Trace kufariki na
mtoto aliyezaliwa, kupoteza mzazi wake. Mke wa Dkt. Gumbo hakujali utu na
uhai wa mtu, ili mradi lengo lake la kuhakikisha kuwa mimba ile inatoka,
linatimia.
Suala la ukatili katika filamu hii pia, linasababishwa na ushawishi. Hii
inajidhihirisha pale ambapo James anakubali kushawishiwa na mkewe Jesca ili
wamtese Tamala wakati alipokuwa akiishi pamoja nao katika nyumba ya urithi.
Jesca ni wifi mkatili ambaye anamshawishi James afanye ukatili kwa Tamala.
Wote wawili wanamnyanyasa Tamala kwa kumnyima haki za msingi kama
elimu, na anaishia tu kufanya kazi za nyumbani. Pia wakati alipokuwa anaumwa
hawakumjali wala kumpeleka hospitali mpaka alipozimia ndipo walimpeleka
hospitali. Tamala alipopata nafuu alirudi nyumbani akidhani kuwa maisha
yangebadilika lakini haikuwa hivyo. Alipoona kuwa taabu zinazidi na hakuna
dalili za mabadiliko aliamua kuondoka na kwenda kuishi na shangazi yake.
Ushawishi na ukatili wa mawifi katika jamii yetu ya Kitanzania upo na
umekuwa ni tatizo katika kusambaratisha jamii. Filamu hii ya Taswira imeakisi
hali halisi ya mahusiano katika ndoa ambao unasababisha migogoro mbalimbali
katika familia.

Uongozi
Suala la uongozi katika filamu ya Taswira pia, limegusiwa. Katika filamu hii,
uongozi wa kijiji umeonekana ukiwajibika katika kuwasaidia wananchi kutatua
masuala mbalimbali ya kijamii kama vile migogoro na masuala mengine ya
kifamilia na ya kijamii kwa ujumla. Pia uongozi unaozungumziwa katika filamu
hii unasisitiza kufuata na kuheshimu sheria za nchi, hususan sheria za umilikaji
wa ardhi. Hii inajidhihirisha kwa kuwaangalia wahusika Tamala na Baraka
ambao walikwenda kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji kuhusu uharibifu wa
mashamba yao uliofanywa na mifugo. Uongozi huo wa kijiji ulifikia uamuzi
kuwa wafugaji wote walipie fidia ya uharibifu wa mazao uliofanyika. Hii
inaonyesha kuwa uongozi wa kijiji pamoja na maamuzi wanayofanya
yanaheshimiwa na wanakijiji.
Umaskini
Umasikini ni hali ya kukosa mali, ufukara na ukata (TUKI 2004). Umaskini ni
miongoni mwa matatizo makubwa yanayozikumba nchi zinazoendelea.
Kutokana na kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo, umasikini
unajitokeza kwa kiasi kikubwa na kuathiri maisha ya watu. Watanzania walio
wengi ni masikini sana mpaka kiasi cha kushindwa kumudu maisha yao na
kuacha urithi wowote wa mali kwa watoto wao (Chiraka 2009:54). Umaskini
umesababisha watu wengi kushindwa kupata huduma muhimu kama elimu,
huduma za kiafya na hata maji. Zipo kazi mbalimbali za sanaa ambazo
zimezungumzia suala la umaskini. Mathalani katika Riwaya ya Shida, Chonya
na Matika wanakutana na hali ngumu ya maisha mpaka wanaamua kwenda
mjini kutafuta maisha. Huko mjini wanakumbana na hali ngumu zaidi mpaka
wanaamua kurudi tena kijijini ambapo wanagundua kuwa elimu ndiyo
mkombozi wa maisha yao. Vilevile katika tamthiliya ya Ngoswe Kitovu cha
Uzembe dhamira ya umaskini ni mojawapo ya dhamira zilizojadiliwa. Hali hii
inajidhihirisha kwa kuangalia malazi pamoja na mavazi ya wahusika.

Katika filamu ya Taswira suala la umaskini limejitokeza kwa kuangalia maisha


ya Tamala na Trace. Umaskini wa familia ya akina Trace unajidhihirisha kwa
malazi, yaani nyumba yao waliyokuwa wakiishi ilikuwa ni ya udongo. Pia
maisha yao yalikuwa duni kiasi ambacho Tamala alishindwa kumlipia Trace ada
ya chuo kikuu. Hali hii ilimlazimu Trace kutafuta ufadhili kwa watu wengine
ambapo ilimsababishia kupata mimba na hatimaye kufa. Umaskini unaweza
kusababisha watu kujiingiza katika mambo ambayo yanahatarisha maisha yao.
Kwa mfano wapo wasichana waliojiingiza katika masuala ya mapenzi ili
waweze kupata fedha za kujikimu. Hali hiyo huwaweka katika mazingira
hatayarishi ya kuweza kupata ugonjwa wa UKIMWI na madhara mengine.
Migogoro katika Filamu ya Taswira
Migogoro ni kipengele kimojawapo kinachotumika kuelezea maudhui.
Kutokana na mivutano inayotokea katika kazi ya fasihi, yanazuka matukio
ambayo yanasaidia katika kupata maudhui. Wamitila (2003) anaeleza kuwa
mgogoro hutumiwa kurejelea mvutano unaokuwako kati ya mhusika mmoja na
mwingine katika kazi ya fasihi au katika akili ya mhusika mmoja. Migogoro ni
sehemu muhimu katika msuko wa kazi ya fasihi na huchukua sehemu kubwa ya
kazi hiyo. Mgogoro hujitokeza kwa njia mbalimbali. Senkoro ( 1982:4 )
anaeleza kuwa katika kazi ya fasihi kuna migogoro kati ya wahusika, ama
vikundi vya wahusika, familia zao, matabaka yao na kadhalika. Migogoro
yaweza kuwa ya kiuchumi, kiutamaduni au kisiasa. Halikadhalika kuna
migogoro ya kinafsia ambayo inatokea katika nafsi ya mhusika.

Katika filamu hii ya Taswira ipo migogoro mbalimbali iliyojitokeza. Kwa mfano
kuna mgogoro kati ya wakulima na wafugaji. Chanzo cha mgogoro huu ni
wafugaji kuingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima na kusababisha
uharibifu. Baada ya wakulima kuona hali hiyo, wanatoa taarifa katika serikali ya
kijiji na inaamuliwa kwamba wafugaji walipe fidia ya uharibifu wote
uliofanyika. Katika jamii ya Kitanzania ipo migogoro ya ardhi kati wa wakulima
na wafugaji. Kwa mfano, kuna mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na
wafugaji wa Kimasai Arusha na Morogoro kiasi cha serikali kuingilia kati kwa
kuwahamishia baadhi ya wafugaji katika mikoa mingine.

Mgogoro mwingine ambao unajitokeza katika filamu ya Taswira ni ule wa


mirathi uliosababishwa na dhuluma ya mali ya urithi kati ya ndugu wawili,
James na Tamala. Suala hili linajidhihirisha pale ambapo James anamdhulumu
Tamala urithi walioachiwa na baba yao. James alitumia mali ya urithi vibaya
kwa kujinufaisha yeye pamoja na mke wake bila kumjali mdogo wake (Tamala).
Hali hii inaonyesha jinsi mali ya urithi inavyoweza kuleta mgogoro katika
familia. Hata hivyo, mwisho wa James haukuwa mzuri kwani alifilisiwa mali
zote na mkewe (Jesca) na kumuacha hana kitu. Kutokana na hali hiyo James
alishikwa na ugonjwa na kuamua kurudi kijijini alikokuwa akiishi Tamala na
kumuomba msamaha. Tamala kutokana na huruma zake alimsamehe kaka yake.
Hali hii inaungwa mkono na usemi kuwa, “Damu nzito kuliko maji.”

Mgogoro mwingine mkubwa unaojitokeza katika filamu ya Taswira ni kati ya


Trace na familia ya Dkt. Gumbo. Suala la ufadhili wa Trace hatimaye lilizua
mtafaruku mkubwa kati wa watu wa familia ya Dkt. Gumbo. Uhusiano wa
kimapenzi kati ya Dkt. Gumbo na Trace ambao ulisababisha Trace kupata
ujauzito na kuleta mgogoro kati Dkt. Gumbo na mkewe. Matokeo yake Trace
alikufa. Hii inaonyesha jinsi migogoro ya kimapenzi inavyoweza kuwa na athari
kubwa katika maisha ya watu. Trace anapewa vidonge vya kutoa mimba na Mke
wa Dkt. Gumbo na hatimaye anafariki. Katika jamii ya Kitanzania ipo migogoro
mingi kati ya makundi mbalimbali ya watu. Migogoro hii yaweza kuwa na
vyanzo mbalimbali kama ukosefu wa haki, uonevu, mapenzi, wivu, tofauti za
kiuhusiano na usaliti.

Falsafa ya Mtunzi katika Filamu ya Taswira


Senkoro (1980) anaeleza kuwa falsafa hubainisha msimamo ama mtazamo wa
msanii kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Msimamo ndio unaoweza
kuwatofautisha wasanii mbalimbali. Katika filamu ya Taswira falsafa ya mtunzi
ni kuhusu maisha na changamoto zake. Mtunzi anaona kuwa katika kukabili
matatizo hayo binadamu anakumbana na vikwazo mbalimbali ambavyo vinazuia
mafanikio. Kwa mfano vikwazo katika kutafuta elimu vinatokea kwa hiyo ni
vyema kufanya uchaguzi sahihi na kutumia njia sahihi ya kutatua matatizo ili
kufikia malengo yaliyokusudiwa. Pia binadamu ana taswira mbalimbali katika
akili yake. Katika kutimiza hayo binadamu hujiwekea mafanikio kwa asilimia
mia moja bila kujali kuhusu changamoto au vikwazo ambavyo vinaweza
kutokea. Kwa mfano, Trace alijenga taswira akilini mwake kuwa atafanikwa
kupata elimu lakini haikuwa hivyo. Kwa ufupi falsafa ya mtunzi hapa
inaonyesha kuwa maisha ni safari ndefu na yana changamoto zake.

Ujumbe katika Filamu ya Taswira


Katika filamu ya Taswira ujumbe unaopatikana ni kuwa ingawa kuna mitihani
mingi katika kufikia malengo ya kimaisha tusikate tamaa.. Pia katika kufikia
malengo ya baadaye inabidi kuwasikiliza waliotutangulia, yaani wazazi hasa
wanapotoa ushauri; kwani “asiyesikia la mkuu huvunjika guu”. Mfano mzuri ni
Trace ambaye hakusikia maneno na ushauri wa mama yake kuhusu kuridhika na
hali ya maisha waliokuwa nayo. Kushindwa kufanya hivyo kulimfanya Trace
hatimaye kufariki.

Katika sehemu hii, tumeona dhamira mbalimbali zikijadiliwa pamoja na falsafa


na ujumbe. Sehemu inayofuata, dhamira mbalimbali, falsafa na ujumbe
vitajadiliwa.

Dhamira katika Filamu ya Vita vya Ushindi

Vita vya Ushindi ni miongoni mwa filamu za Kiswahili ambazo zinaonyesha


jinsi watu na jamii ya Kitanzania wanavyoishi katika mazingira tofautitofauti.
Filamu hii inaonyesha migogoro mbalimbali inayotokea ambayo chanzo chake
kikuu ni uzazi na imani. Zipo imani za kijadi na zile za kidini. Katika kutatua
migogoro hiyo watu wanategemea imani hizo. Watu wanaona kwamba imani
zao huweza kutatua matatizo mbalimbali ambayo yanawakumba watu.
Miongoni mwa dhamira katika filamu hii zitajadiliwa katika kipengele cha 5.5.1
hadi 5.5.8.

Uzazi na Ndoa

Uzazi ni kielelezo cha kuwepo na kukua kwa jamii ya mwanadamu popote pale
ulimwenguni. Ijapokuwa uzazi ni kitambulisho kikubwa cha kuwepo (uhai) na
kukua kwa jamii, mtazamo juu ya jambo hili kwa jamii moja au nyingine
unaweza kufanana au kutofautiana kulingana na mazingira ya jamii. Katika
ontolojia ya Kibantu, uzazi huchukuliwa kama kitu muhimu sana katika asili ya
Wabantu na kinachoweza kuleta mshikamano katika ndoa na ndani familia. Kwa
Wabantu, uzazi ni suala zito na linaheshimiwa na kuthaminiwa katika jamii zao.
Katika jamii za Wabantu kuna sherehe mbalimbali zinazofanywa ambazo lengo
na madhumuni yake ni kuuenzi uzazi. Kwa mfano, sherehe za kuzaliwa na
kumpa mtoto jina zinaashiria kusherehekea kuongezeka kwa ukoo. Hivyo
wanajamii wanasherehekea kwa lengo la kumkaribisha mwanafamilia mpya
katika jamii (Mbiti 1969).

Hali kadhalika, katika sherehe za jando na unyago lengo mojawapo kubwa la


kuwafunda vijana huwa ni kuwaeleza umuhimu wa uzazi katika jamii zao. Hii
ina maana kwamba msisitizo kwa vijana hao huwa ni suala zima la ndoa ambalo
ndilo linalounganisha mwanamke na mwanaume hatimaye kupata watoto ambao
wataendeleza ukoo na jamii yao kwa ujumla. Hata katika ibada za matambiko
yanayofanywa na jamii nyingi za Kibantu zinahusu uzazi kwa maana kwamba
huombwa mizimu kuuendeleza ukoo wao kwa kuwapa kizazi na waondokane na
laana ili ukoo uendelee (Mbiti 1969). Hivyo, ibada kama hizo zilizotajwa,
zinazofanywa na jamii za Kibantu kwa namna moja au nyingine, zinahusishwa
moja kwa moja na suala zima la uzazi.
Mbiti anaendelea kueleza kuwa baadhi ya jamii za Kiafrika wanaamini kuwa
raha ya ndoa ni kupatikana kwa watoto. Na ndoa yenyewe hutambulika pale tu
mwanamke atakaposhika mimba na kuzaa. Mwanamke anaposhindwa kuzaa
watoto hata kama atakuwa na sifa nyingine nzuri, nyumba hiyo hujawa na
huzuni na hujiona kama wana mkosi na laana kutoka kwa wahenga wao. Na
mwanamke anapokosa uzazi huaminika kuwa ametenda kosa kubwa sana.
Kutokana na mtazamo wa Kiafrika ni kwamba suala la uzazi lina uhusiano wa
moja kwa moja na ndoa na mapenzi. Watu wanapooana wanatarajia kupata
watoto ambao ndiyo wanakuwa kiungo cha familia yao. Pia kutokana wa
mtazamo wa jamii ya Kitanzania ambayo ni miongoni mwa jamii za Kibantu ni
kuwa, watu wanapooana lazima wazae. Lakini mwanamke ndiye huonekana
kiini au mlengwa wa kuleta matunda. Kunapotokea matatizo ya uzazi katika
familia mtu wa kwanza kulaumiwa ni mwanamke na siyo mwanaume.
Mwanamke huanza kupata manyanyaso kutoka kwa ndugu upande wa mume,
akiwemo mama mkwe na mawifi. Hali hii imesababisha kusambaratika kwa
ndoa nyingi hasa kutokana na shinikizo kutoka kwa wazazi na ndugu wengine.

Katika filamu ya Vita vya Ushindi suala la uzazi, mapenzi na ndoa


limesawiriwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwaangalia wahusika Fred na Stella
katika maisha yao ya ndoa. Wahusika hawa wawili wamekuwa na mapenzi ya
kweli kwa muda mrefu. Japokuwa Stella alishindwa kupata mtoto kwa muda
mrefu lakini mume wake alivumilia na alionyesha kuridhika na hali hiyo.
Kutokana na shinikizo kutoka kwa wazazi wa Fred, maisha ya Fred na Stella
yalibadilika kutokana na tatizo la uzazi alilokuwa nalo Stella. Wazazi wa Fred
walimshinikiza Fred amwache Stella na amuoe Jane. Wazazi walitawaliwa na
mtazamo wa Kiafrika kuwa mwanamke akishaolewa lazima azae na si
vinginevyo. Tatizo hili la kutokuzaa kwa Stella limezusha mgogoro mkubwa
kati ya familia ya Fred na familia ya Stella. Hii inaonyesha jinsi jamii
inavyolichukulia suala la uzazi kuwa ni muhimu hasa katika ndoa.

Pia inaonyesha nafasi ya mwanamke mwenye matatizo ya uzazi na jinsi


alivyochukuliwa katika jamii kwamba anaonekana kuwa chanzo cha matatizo
hayo. Hata hivyo, shinikizo hilo la Fred kumwacha Stella na kuoa mke
mwingine halikufanikiwa kwa sababu Stella alikuwa mshika dini. Maombi yake
yalimsaidia na hata hatimaye alipata ujauzito na kufanikwa kupata mtoto wa
kiume.

Kwa mtazamo wa Kiafrika, watu wengi huona kuwa ili kuishi pamoja katika
ndoa, kuzaa ni lazima. Wanasahau upande mwingine kuwa kuzaa ni majaliwa ya
Mwenyezi Mungu. Hapa inaonyesha kuwa katika jamii za Kibantu uzazi ni
suala muhimu, na ndio maana katika filamu hii Stella alipatwa na misukosuko
kutokana na tatizo la kutozaa. Hii inaakisi hali halisi ya maisha ya watu katika
jamii ya Kitanzania kwani wapo wanawake wengi wenye matatizo ya uzazi
ambao wananyanyasika katika ndoa zao. Hii imewasababishia matatizo ya
kisaikolojia hatimaye kuvunjika kwa ndoa zao.

Ushirikina na Uganga
Suala hili limejitokeza katika tamthilia kadhaa, mathalani, tamthilia ya
Emmanuel Mbogo, Ngoma ya Ng’wanamalundi na Ibrahim Hussein, Kinjekitile.
Kwa ujumla, ushirikina na uganga kama itikadi za jadi katika tamthiliya hizi
zinasawiriwa kama amali muhimu za jamii zifaazo kutumiwa kutatua baadhi ya
matatizo ya kimaisha. Uchawi na itikadi za ushirikina, vilevile ni tatizo sugu
lenye kukwamisha maendeleo (Mulokozi 1996:210). Zipo imani za aina
mbalimbali lakini imani zinazozungumziwa hapa ni imani za kijadi ambazo
zinahusisha ushirikina au nguvu za mizimu na miungu wengine. Nguvu hizi
kama ilivyoelezwa hapo awali hutumika katika kutatua matatizo mbalimbali ya
kijamii na watu wanaziamini kuwa zinafanya kazi.

Katika filamu ya Vita vya Ushindi, imani za kijadi yaani ushirikina limejitokeza
kwa kiasi kikubwa. Hii inajidhihirisha kwa kumwangalia Mama Fred, Mama
Jane, Jane na mganga Masolosolo. Wahusika wanaamini kuwa nguvu hizi
zinafanya kazi hasa pale walipotaka kuiharibu ndoa ya Fred na Stella kutokana
na tatizo lake la kutozaa. Mama Fred anaona kuwa njia pekee ya kumuondoa
Stella kwenye ndoa ni kutumia ushirikina na uganga. Katika kutimiza hilo
Mama Fred anaamua kwenda kwa mganga ambaye anawapatia dawa ambazo
wanaamini zingefanya kazi. Katika kudhihirisha ushirikina na uchawi wao,
Mama Fred anamtuma Jane kuchukua nguo za ndani za Stella ambazo
zilianikwa kwenye kamba ili waweze kuzifanyia uchawi. Jane anafanya hivyo
na anafanikiwa kuzipata. Hii inaashiria kwamba uchawi unaweza kufanywa kwa
kupitia nguo za mtu. Nia yao kubwa ilikuwa kutaka kumwachisha ndoa yake.
Pia, katika ushirikina wao Mama Fred na Jane wanadiriki kuamka usiku na
kwenda kuwanga chumbani kwa akina Stella. Kutokana na kushika dini, Stella
alikuwa na nguvu za kuweza kupambana na uchawi. Alipata uwezo wa kuwaona
wakati wakiwa wanawanga usiku na kumwamsha mumewe ili aweze
kushuhudia.

Katika jamii wapo watu ambao wanategemea nguvu za uchawi na uganga katika
kutatua matatizo yao mbalimbali. Jamii nyingi hasa zile ziishizo vijijini na
maskini zinaamini sana ushirikina. Pia mijini ushirikina upo kwani baadhi ya
watu wenye nyadhifa zao ambazo wanaamini kuwa nguvu za sihiri zinaweza
kuwasaidia kupata madaraka au wasiondolewe katika madaraka. Hudiriki
kusafiri safari ndefu kwenda kutafuta nguvu za sihiri ili waweze kudumu katika
madaraka. Mbali na viongozi, wapo watu wa kawaida ambao hutumia uganga
katika kutatua matatizo kama magonjwa, mahusiano ya kimapenzi na kadhalika.
Imefikia hatua mpaka waganga wanajinadi na kujitangaza kwenye magazeti na
mabango ili kuvutia biashara. Kwa hiyo, hii inaonyesha kuwa masuala ya
uganga yamefanywa kama shughuli ya kujipatia pesa. Lakini mwishoni
inaonyesha kuwa nguvu hizo hazidumu kwani watu wanaotegemea sana nguvu
hizi mwisho wake huanguka (hushindwa).

Usaliti

Usaliti ni miongoni mwa dhamira zinazojitokeza katika kazi mbalimbali za


fasihi.

Usaliti ni hali ya kwenda kinyume na makubaliano yaliyofanyika hapo awali


kati

ya makundi mawili au pande mbili. Usaliti unatokea katika nyanja mbalimbali


kama siasa, mapenzi, michezo na uhusiano kwa ujumla. Zipo kazi mbalimbali
ambazo zimegusia suala la usaliti. Kwa mfano, katika Mashairi ya Chekacheka
(1995), Mvungi anaelezea suala la usaliti wa viongozi katika shairi la Taifa
Wamelizika. Anaeleza kuwa baadhi ya viongozi ni wasaliti wa wananchi kwani
hawajali maslahi ya wananchi bali yao binafsi.

Katika filamu ya Vita vya Ushindi usaliti unaojitokeza ni usaliti wa kimapenzi


yaani usaliti katika ndoa. Hii inajidhihirisha kwa kumwangalia mhusika Fred
jinsi alivyoweza kumsaliti mkewe kwa kubadili uelekeo au msimamo wake wa
awali kuhusiana na suala la kudumisha mapenzi na ndoa kwa mke wake Stella.
Usaliti huu ulichochewa na mama yake Fred ambaye alikuwa akimpiga vita
Stella kwa sababu alikuwa hazai. Mwanzoni kabisa inaonyesha kuwa Stella na
Fred walikuwa na mapenzi ya kweli na walikubaliana kuishi bila kujali tatizo la
uzazi. Lakini baadaye anaonekana akibadili nia yake ya na kuanza kumnyanyasa
Stella. Suala la usaliti na kubadili nia katika ndoa linatokea katika jamii yetu ya
Kitanzania. Wapo wanaume wengi ambao wamesaliti ndoa zao kutokana na
sababu mbalimbali. Sababu hizo zaweza kuwa tabia au hulka binafsi za
wanaume kuwakwa na tamaa, wanawake kutowajali waume zao, matatizo ya
uzazi hasa kwa upande wa mwanamke, ukosefu wa maadili na ulevi. Tatizo la
uzazi katika baadhi ya familia limewafanya wanaume kuwaacha wake zao na
kwenda kutafuta wanawake wengine nje ya ndoa ambao wanadhani kuwa
wanaweza kuwazalia watoto. Usaliti umepelekea wanaume wengine kuwa na
ndoa za mitala na uhusiano wa siri na hata kupata magonjwa ya zinaa kama
UKIMWI na kuhatarisha ndoa zao kwa ujumla. Hivyo, usaliti katika ndoa
unaweza kuwa na madhara makubwa. Mashindano kati ya mke mkubwa na mke
mdogo (wake wenza), yanaweza kutokea pale ambapo mmojawapo anaweza
kufanya mambo ya kishirikina ili waweze kuwa na sauti zaidi kwa mume wao.
Hali hii huweza kuleta madhara kwa familia nzima. Vilevile wapo wanawake
ambao wanasaliti ndoa zao kwa kukosa auminifu na kuwa na uhusiano na
wanaume wengine.

Unyanyasaji wa Kijinsia
Hili ni suala linalojitokeza kwa kiasi kikubwa katika kazi mbalimbali za fasihi
kama vile riwaya, tamthiliya na ushairi. Watunzi wanajaribu kuonyesha hali duni
ya mwanamke katika jamii ya sasa ili kutafuta sababu ya hali hiyo na
kupendekeza ufumbuzi. Baadhi ya waandishi wa tamthiliya wanaogusia suala
hilo ni Muhando, katika Nguzo Mama, Machozi ya Mwanamke, Mulokozi,
katika Mukwawa wa Uhehe, Mazrui, katika Kilio cha Haki na Ebrahim Hussein
Kwenye Ukingo wa Thim. Unyanyasaji wa kijinsia ni suala ambalo linatokea
sana katika jamii zetu za sasa na limekuwa ni chanzo cha matatizo kama
mafarakano katika familia na hata ulemavu. Kwa mfano Jarida la FEMA
(2010:11) linaeleza kuwa unyanyasaji wa kijinsia ni tendo lolote lenye mtazamo
wa jinsia linaloweza kumsababishia mtu adha au kero, madhara na mateso ya
kimwili, kisaikolojia na kingono.

Katika filamu ya Vita vya Ushindi, unyanyasaji wa kijinsia unajitokeza kwa


kumwangalia mhusika Stella jinsi alivyokuwa akinyanyaswa na Fred baada ya
kushinikizwa na wazazi wake amwache. Stella alinyanyaswa kutokana na tatizo
la kukosa uzazi. Fred anadiriki kumwambia mkewe kuwa kama anaona mambo
yamebadilika ni vyema afungashe vitu vyake aondoke aende kwao. Majibu haya
kutoka kwa Fred yanamuumiza sana Stella na kumfanya kukosa raha.

Hii inaonyesha unyanyasaji wa kijinsia kwa kutishia kumwacha mwanamke ni


kumnyanyasa kisaikolojia. Usemi huu unaweza kulinganishwa na ule wa
kwenye Wimbo wa Lawino (1975) pale Ocol anapomwambia Lawino,
“Mwanamke kaa kimya, fungasha vitu vyako uondoke” (uk. 121). Wimbo huu
wa Lawino ulioandikwa na Okot p’ Bitek unaonesha jinsi Ocol alivyokuwa
akimdharau mkewe kuwa hajasoma na ni mshamba kwa hiyo hafai kuwa mke
wake. Hii inaonyesha dharau, na unyanyasaji wa kijinsia. Hii ilisababishwa na
Ocol kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa nje ambaye ni
Clementine.

Katika Filamu ya Vita vya Ushindi Stella ananyanyasika, lakini anaonyesha


ujasiri kwa kuwa anamwamini Mungu na anaendelea kufanya maombi juu ya
suala hilo. Katika jamii ya Kitanzania suala hili la unyanyasaji linatokea kwa
kiasi kikubwa na wanawake wengi wamekuwa wakiathirika kutokana na
unyanyasaji wanaoupata katika ndoa. Wanaume ndiyo wamekuwa chanzo cha
unyanyasaji na dharau hasa pale wanapokuwa na uhusiano nje ya ndoa, tabia
inayopelekea wawe wadanganyifu na kuwadharau wake zao. Unyanyasaji huu
umeleta matatizo katika ndoa kama kufarakana na kutengana. Pia umeweza
kusababisha maumivu na uelemavu hasa pale unyanyasaji wa kipigo unapotokea
kwa wanawake.

Ujasiri na Uvumilivu
Kutokata tamaa, ujasiri na uvumilivu kunajitokeza kwenye kazi mbalimbali za
fasihi. Kwa mfano katika riwaya ya Watoto wa Mama Ntilie, mhusika Mama
Ntilie anachorwa kuwa mvumilivu, jasiri na asiyekata tamaa ya maisha. Hii
inajidhihirisha kwa jinsi anavyoweza kuvumilia matatizo ya ulevi wa mume
wake bila kukata tamaa. Anaamua kufanya biashara ndogondogo kwa lengo la
kutokomeza umaskini unaoikabili familia yao. Katika riwaya hii pia Kurwa ni
mmoja wa wahusika wavumilivu na jasiri katika kuyakabili matatizo.

Katika filamu ya Vita vya Ushindi, dhamira hii inajidhihirisha kwa kumwangalia
mhusika Stella ambaye anaonyesha ujasiri katika kupambana na changamoto
ambazo zinamkabili. Mbali na kunyanyaswa kutokana na kutozaa, Stella
hakukata tamaa, aliendelea kumuomba Mungu akitegemea kuwa atamsaidia.
Stella aliendelea kuwa mnyenyekevu na mvumilivu mbali na matatizo na
manyanyaso yote aliyoyapata katika ndoa yake kutoka kwa wazazi wa Fred na
Fred mwenyewe. Alivumilia mpaka Mungu (kwa imani yake) alipomjalia kupata
mtoto. Wanawake wengi wamekuwa wakipata matatizo haya katika ndoa zao
lakini wamekuwa wavumilivu ili waweze kutunza watoto na familia kwa
ujumla.

Starehe
Starehe ni hali ambayo mtu au watu hujiliwaza kwa kufanya matendo ambayo
wao hufikiri wanaweza kupata raha au faraja ya namna fulani. Zipo starehe za
aina mbalimbali kama kutumia vinywaji, kujihusisha na masuala ya mapenzi,
kushiriki katika michezo mbalimbali na kadhalika. Starehe hutegemea mtazamo
wa mtu mwenyewe kuwa ni kitu gani anapenda. Kitu fulani kinaweza kuwa
starehe kwa mtu mmoja na kuwa karaha kwa mtu mwingine. Katika filamu hii
ya Vita vya Ushindi suala la starehe linajidhihirisha kwa kumwangalia Fred na
marafiki zake ambao wamekaa baa wakinywa pombe na wanawake
wanaoendesha ukahaba.

Starehe zao hizi zinasababisha mpaka kutafutiana wapenzi. Kwa mfano, Rich
anamtafutia Fred mwanamke wa kustarehe naye wakati anajua fika kuwa Fred
ana mke wake. Fred anaingia katika mkumbo wa kujihusisha kimapenzi na
mwamke wa nje, yaani Wema, kutokana kuchanganywa na wazazi wake kuwa
Stella hafai. Matokeo yake ni kwamba waliishia kufanya starehe na kusahau
familia zao. Kwa kuwa Fred alikuwa ni mcha Mungu hakutarajiwa kunywa
pombe na kujihusisha na masuala ya mapenzi nje ya ndoa. Kwa mtazamo huu
Fred anachukuliwa kuwa ametenda dhambi kwa kukiuka amri za Mwenyezi
Mungu ambazo zinakataza watu kutumia kilevi cha aina yoyote, kutamani na
kuzini na mke wa mtu na kadhalika.

Kwa ujumla starehe kupita kiasi hasa unywaji wa pombe, umekuwa na madhara
makubwa katika familia mbalimbali. Ulevi umefanya watu kuwa maskini
kupunguza kipato cha familia na kushindwa kuhudumia familia ipasavyo. Ulevi
pia unaweza kusababisha kupoteza maisha kutokana na kunywa pombe kali
kupita kiasi. Madhara mengine ni kama kuvunjika kwa familia, umalaya, ukatili
na unyanyasaji, ukosefu wa maadili katika familia, na kutokuwajibika. Katika
jamii ya Kitanzania matukio kama unywaji wa pombe, wanaume kufanya
uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yanatokea na kuathiri maendeleo ya jamii
kwa ujumla. Zipo familia zilizosambaratika kutokana na athari za starehe za
kupita kiasi. Starehe pia zimepelekea watu kuathirika na magonjwa yasiyopona
kama UKIMWI.
Utoaji wa Mimba na Mimba Nje ya Ndoa
Kama ilivyoelezwa hapo awali katika filamu ya Taswira, dhamira hii pia
inajitokeza katika filamu ya Vita vya Ushindi. Hii inajidhihirisha pale ambapo
mchumba wa John anamlazimisha John waitoe mimba. John anaonekana
kutokukubaliana na suala hilo. Wanaamua kumuona daktari ambaye anawaeleza
kuwa kutoa mimba ni hatari. Uamuzi wa kwenda kumuona daktari unaonyesha
jinsi John alivyokuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na athari za utoaji
mimba. Pia inaonyesha jinsi baadhi ya madaktari wanavyoweza kutoa ushauri
mzuri kwa kuzingatia maadili ya kazi zao. Ushauri wenye busara huepusha
madhara kwa watu hasa wasichana wanaotaka kutoa mimba.

Kama ilivyoelezwa hapo awali katika uchambuzi wa filamu ya Taswira kuwa


suala la utoaji mimba kwa wasichana ni tatizo katika jamii yetu ya Kitanzania.
Wasichana wengi wanadiriki kutoa mimba bila kujali athari zake. Hii yaweza
kuwa ni kwa sababu za kiuchumi au kutelekezwa na wapenzi wao. Pia
yawezekana kuwa vitendo vya utoaji mimba vinatokana na mtazamo kwamba
mimba nje ya ndoa ni aibu. Hivyo wasichana hutoa mimba ili kukwepa aibu
hiyo bila kujali kuwa wanahatarisha maisha yao. Filamu ya Vita vya Ushindi
inatoa mwongozo mzuri kuhusiana na suala la utoaji mimba kwa kuzingatia
ushauri wa daktari ambaye anakataza na kukemea kitendo hicho kwa kuonyesha
madhara yake. Kwa upande wa madaktari, utoaji mimba waweza kuwa chanzo
cha kuwaingizia kipato cha ziada. Hii inashadadiwa na matatizo ya kiuchumi na
ukosefu wa maadili ya udaktari kwa ujumla.

Dini, Imani na Maadili

Suala la dini, imani na maadili limezungumziwa na waandishi mbalimbali wa


kazi za fasihi kama vile riwaya na mashairi. Kwa mfano, kazi za Siku ya
Watenzi Wote, Inkshafi, Utenzi wa Mwanakupona na Malenga wa Mvita
zimeelezea nafasi ya dini katika maisha ya binadamu. Kufuata dini kunaonekana
kama njia inayoweza kumkomboa mwanadamu dhidi ya tamaa, ufisadi, ubinafsi
na matatizo mengi ya maisha yanayoikumba jamii. Dini inaonekana kuwa
suluhisho la maisha na inatoa mwangaza juu ya tabia zinazofaa kufuatwa kama
kuaminiana, kuheshimiana, kupendana na kuwa na nia safi. Dini ina lengo kuu
la kumfanya binadamu awe mwema zaidi na kuwa na maadili mazuri (Njogu na
Chimerah 2008: 24).

Kwa upande wa tamthiliya, dini kama asasi ya kijamii imejitokeza katika


tamthiliya kama Aliyeonja Pepo na Mkwawa wa Uhehe. Watunzi wa tamthiliya
hizi wanaonyesha kuwa hakuna tamthiliya hata moja iliyokanusha kuwepo kwa
Mungu na mitume wake (Mulokozi 1996: 209). Katika filamu ya Vita vya
Ushindi, dini iliyozungumziwa ni dini ya Kikristo. Dini hii inaonekana kuwa
suluhisho la matatizo ya maisha na inatoa mwangaza juu ya tabia njema
zinazofaa kufuatwa. Pia dini inaonekana kuleta kuaminiana, kusameheana na
kuungana na vizazi viliyopita.

Dini ya Kikristo, inajidhihirisha kwa kuwaangalia wahusika Stella na Fred


ambao wanaonekana wakisoma Biblia na kufanya maombi kwa kutegemea
sana nguvu za Mungu. Kwa mfano, Stella anapopata matatizo ya kukosa amani
katika familia, anafanya maombi na Mungu anasikia sala zake. Pia Stella katika
tatizo lake la uzazi anamtegemea Mungu kwa maombi na hatimaye anapata
mtoto anayemwita Jacob. Stella anaamini kwamba ukiwa na imani kwa Mungu
yote yanawezekana. Katika jamii ya Kitanzania zipo dini mbalimbali kama vile
dini ya Kikristo, Kiislamu na imani za kijadi na watu wanaamini kuwa Mungu
yupo na anasaidia watu katika shida mbalimbali. Wapo watu wengi
wanaotegemea maombi wakati wanapopatwa na matatizo mbalimbali . Kwa
mfano, katika makanisa na misikiti kuna vipindi vya kuombea mapepo, kuomba
mvua, amani, kuombea wagonjwa na matatizo mengine.

Migogoro katika Vita vya Ushindi


Migogoro katika jamii au makundi ya watu haiepukiki. Migogoro hiyo huweza
kuleta madhara au maendeleo. Ila kwa kiasi kikubwa migogoro huleta
mafarakano katika makundi mbalimbali ya jamii. Katika filamu hii, chanzo
kikubwa cha migogoro hii ni suala la uzazi. Stella ni mhusika ambaye alikuwa
na tatizo la kutokuzaa. Familia ya upande wa Fred ilimnyanyasa Stella kutokana
na tatizo hilo. Mgogoro huu ulitokana na shinikizo kutoka kwa wazazi.
Mwishoni inaonekana kuwa mgogoro huu ulipata muafaka kwa Stella
kufanikiwa kupata mtoto. Mgogoro mwingine ni mvutano kati imani za kijadi na
nguvu za kiroho (Ukristo). Nguvu za imani ya Kikristo ndio inabeba hata jina la
filamu yenyewe, Vita vya Ushindi, ikiwa na maana mapambano ya pande mbili
kati ya Ukristo na imani za uchawi na ushirikina. Stella na Fred wanawakilisha
upande unaofuata nguvu za kiroho wakati Jane, mama Jane na mama Fred
walifuata (imani za ushirikina na uganga). Katika mgogoro huu upande
uliokuwa unafuata nguvu za kiroho yaani dini ya Kikristo ulishinda. Hii
inaonyesha jinsi nguvu za Mungu zinavyoweza kushinda ushirikina na uganga
hivyo kuwafanya waganga kuonekana waongo.

Falsafa ya mtunzi katika filamu ya Vita vya Ushindi


Njogu na Chimerah (1999:48) wanaeleza kuwa mwandishi au mtunzi wa kazi
ya fasihi husimulia tajiriba mbalimbali ambazo zimemkumba au zimeigusa jamii
yake. Kwa hiyo, kazi ya fasihi haitungwi kwa kujistarehesha tu, bali huakisi hali
ya maisha ya jamii fulani. Baadhi ya waandishi huongozwa na msimamo wa
kinadharia ambao huonyesha falsafa yao ya maisha na pia kazi zao zinaathiriwa
na mazingira yaliyomlea na kumkuza. Kwa mfano, mwandishi aliyekulia katika
mazingira ya dini atabainisha falsafa yake katika mazingira ya kidini. Katika
filamu ya Vita vya Ushindi mtunzi ameegemea kwenye falsafa ya maisha
hususani, nafasi ya dini na imani za kijadi. Mtunzi anaona kuwa dini katika
jamii ina nafasi kubwa na muhimu katika kutatua matatizo mbalimbali ya
maisha. Kwa upande, mwingine mtunzi ameongozwa na Ontolojia ya Kibantu
kwa kuhusisha na kuonyesha masuala ya uzazi na nafasi ya imani za miviga na
sihiri katika jamii. Msanii anataka kutuonyesha kuwa jamii za Kiafrika
huyachukulia maisha kwa uasilia.

Ujumbe katika Filamu ya Vita vya Ushindi

Ujumbe katika filamu hii ya Vita vya Ushindi ni kuwa watu wategemee nguvu
za

Mungu kupitia dini, katika kutatua matatizo yao ya maisha na siyo kuegemea
nguvu za sihiri (ushirikina na uganga). Mungu ndiye muweza wa kila jambo, na
nguvu zake zinatenda kazi kuliko nguvu za sihiri. Pia filamu hii inatufunza
kuwa subira yavuta heri. Kuvumiliana katika masuala ya ndoa na uzazi ni
muhimu na siyo kumnyanyasa mwanamke. Pia wazazi wanaaswa kuwa wasiwe
na tabia ya kuingilia ndoa za watoto wao wanapoona kuna tatizo la uzazi kwani
Mungu ndiye anayewajalia au kutokuwajalia watu kupata watoto.

Hitimisho

Filamu ya Taswira na Vita vya Ushindi. Imebainika kwamba kuna dhamira


radidi au motifu ambazo zimejitokeza katika filamu zote mbili. Hii ni pamoja na
motifu ya safari na msako wa kutafuta maisha bora; suala la mimba nje ya ndoa
na suala la utoaji mimba, starehe, unyanyasaji wa kijinsia na nafasi ya
mwanamke. Kufanana kwa dhamira hizi kunaashiria kwamba filamu hizi
zimeakisi masuala mbalimbali ambayo yanatokea katika jamii na pia inaonyesha
kuwa matatizo hayo ni sugu katika jamii ya Kitanzania na bado hayajatafutiwa
ufumbuzi thabiti.

Kitendo cha wasanii wa kazi mbalimbali za fasihi kuonyesha masuala ambayo


yanafanana ni uthibitisho kuwa kile kilichosawiriwa kimelenga yale
yanayotokea katika jamii. Kwani ni dhahiri kuwa, wasanii huwa hawajitengi na
jamii katika utunzi wa kazi zao. Hii ni sawa na mtazamo wa Mulokozi (1996)
kuwa fasihi kama kazi ya ubunifu, husawiri vipengele vya maisha, uhusiano na
hisia za watu katika muktadha fulani. Hivyo ndivyo ilivyojidhihirisha katika
filamu hizi mbili. Masuala ya uhusiano, vipengele vya maisha ya watu kama
elimu, migogoro, changamoto mbalimbali, shughuli za kiuchumi na kadhalika
vimegusiwa. Sura hii imechambua maudhui ikizingatia vipengele vya dhamira,
wahusika, mandhari, migogoro, motifu na ujumbe. Kwa kutumia vipengele
hivyo vilivyotajwa, maudhui yameweza kujadiliwa na kueleweka.

Tamthilia

KARIBU KWENYE DARASA LA TAMTHILIYA

CHIMBUKO LA TAMTHILIYA NA HISTORIA FUPI YA TAMTHILIYA


YA KISWAHILI

NA

HERRY WILLIADY MAJUMBENI

Kabla ya mwambao wa Pwani ya Afrika Mashariki kuingiliwa na athari za


kigeni zilizotoka ng'ambo, fasihi ya Kiswahili, kama fasihi nyinginezo za
kiafrika, ilikuwa ni ya kusimuliwa tu (pasi na kuandikwa) na ilikuwa na tanzu
kama vile ngano, sanaa za maonyesho, vitendawili, methali na kadhalika.
Utanzu wa tamthiliya haukuwa na taswira kama iliyokuwanayo sasa, bali
palikuwa na maigizo ambayo yalitolewa mbele ya hadhira kwa minajili ya
kuongoa na kufundisha maadili au hata kutoa sifa kwa vitendo mwafaka vya
wanajamii husika. Baada ya majilio ya wageni (Waarabu na Wakoloni)
maonyesho haya yalianza kubadilika kwa kuingizwa katika maandishi na kuiga
mitindo ya kimagharibi ili kuchukua mkondo wa tamthilia kwa jumla.

Kihistoria, tamthiliya ilianza kwa kutongoa maudhui ya kidini ambayo aghalabu


yalikuwa ni uteuzi wa visa fulani kutoka katika Bibilia Takatifu ili kutoa funzo
fulani. Pindi mabadiliko yalipoendelea kutokea katika maisha ya mwanadamu,
hali hii ilibadilika hadi kuingia katika tamthiliya zilizozingatia maudhui
mengine kama vile vichekesho na tanzia. Peck na Coyle (1984:75),
wanashadidia maoni haya kwa kusema kuwa katika drama ya Kigiriki, wahusika
walikabiliana na matatizo yaliyohusu uhusiano kati ya binadamu na miungu au
Mungu. Katika karne ya kumi na sita (16) hata hivyo msisitizo ulitoka katika
dini na kuingiza masuala ya kijamii, hivyo tamthiliya zikaanza kuzingatia
maadili ya kijamii na kisiasa.

Katika Kiswahili, tamthiliya ya kwanza kabisa kutungwa na


mwafrikanakuchapishwani ile ya Henry Kuria (1957) kwa kichwa cha
Nakupenda Lakini, ambayo ilitungwa katika enzi ya ukoloni, tamthiiya hii
iliigizwa kwa mara ya kwanza mwaka 1954 huko Kenya. Maudhui yake sawa na
tungo nyingine nyingi za wakati huo, yaliegemea zaidi upande wa kufurahisha.
Huu ni mchezo wa kuigiza unaotongoa maisha ya kijamii, lakini maudhui yake
si mazito na hayazingatii hali ya jamii kujisaka na kujitafiti.

Henry Kuria, Kimani Nyoike, Gerishon Ngugi na B.M Karutu ni miongoni mwa
wanafunzi wa mwanzo wa Graham Hyslop waliokuwa wakisoma katika shule
ya Alliance High School. Hyslop ni mwingereza aliyekuwa katika utumishi wa
serikali ya kikoloni nchini Kenya. Hyslop alianzisha kikundi cha maigizo kwa
ajili ya askari waliopigana katika vita ya pili ya dunia, miaka ya 1950 alianza
kutunga michezo ambayo iliigizwa na kikundi chake. Michezo yake ya mwanzo
katika lugha ya Kiswahili ni Afadhali Mchawi (1957), na Mgeni Karibu (1957).
Inasemekana kuwa Mwingereza huyu (Graham Hyslop) ndiye mtu wa kwanza
kuleta tamthiliya kwa lugha ya Kiswahili yenye kufuata kanuni zote za Ki-
Arstotle. Mbali na Henry Kuria, wanafunzi wengine wa Hyslop walioandika
tamthiliya kwa Kiswahili ni Kimani Nyoike aliyeandika tamthiliya ya Maisha ni
Nini mwaka 1955, B.M Karutu Atakiwa Polisi mwaka 1957 na Gerishoni Ngugi
Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi mwaka 1961.

Mulokozi (1996), anadai kuwa kabla ya Graham Hyslop kuchapisha tamthiliya


zake tayari kulikuwa na tathiliya za Kiswahili zilizoandikwa kwanza kabla ya
kuigizwa jukwaani. Katika kutetea hoja yake Mulokozi anamtaja C. Frank na
tamthiliya yake ya Imekwisha iliyochapishwa mwaka 1951, vilevile anadai kuwa
tamthiliya nyingi katika kipindi hiki zilizugumzia masuala ya kidini, ziliandikwa
na kuigizwa tu mashuleni na makanisani, lakini hazikuchapishwa vitabuni.
Mtaala huyu wa fasihi ya Kiswahili anahitimisha hoja yake hii kwa kusema
kuwa hadi tulipopata Uhuru, tamthiliya zote za Kiswahili zilizochapishwa
ilikuwa zimeandikwa na Wakenya. Madai haya yanaugwa mkono na mtafiti wa
utafiti huu.

Kipindi cha Uhuru,Coyle (1984), anadai kuwa, kabla ya miaka ya 1970,


tamthiliya za Kiswahili zilikuwa chache sana, na nyingi kati ya chache hizo
zilikuwa ni tamthiliya tafsiri, kwa mfano Mfalme Edipode, Mabepari wa Venisi,
Julias Kaizari na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Tamthiliya hizi zilitungwa kwa
kufuata kanuni za Ki-Aristotle na zilikuwa katika mtindo wa kishairi, nyingine
zilizotungwa katika hali ya mazungumzo.

Mulokozi (1996), anaeleza kuwa tamthiliya ya Kizungu na zile za vichekesho


ziliendelea kuandikwa na kuigizwa majukwaani. Tamthiliyaandishi ya Kiswahili
ilishika kasi sana kipindi hiki, Ebrahim Hussein na Penina Muhando waliongoza
katika uandishi wa Tamthiliya ya Kiswahili kwa wakati huu. Tamthiliya za
kipindi hiki zilikuwa zikizungumzia masuala mbalimbali kama vile Migongano
ya Kitamaduni ( mfano ‘Wakati Ukuta na Kwenya Ukingo wa Thim’), Matatizo
ya Kijamii (mfano ‘Lina Ubani, Mke Mwenza, Hatia’), Dini (mfano ‘Aliyeonja
Pepo, Maalim, Mukwava wa Uhehe), Ukombozi na Utaifa (mfano ‘Mkwawa
Mhinya, Johari Ndogo, Kinjekitile, Tone la Mwisho, Harakati za Ukombozi’),
Ujenzi wa jamii mpya (mfano, ‘Kijiji Chetu, Nuru Mpya, Giza Limeingia,
Mashetani, Mwanzo wa Tufani, Kilio cha Haki), Uake na matatizo ya Kijamii
(mfano, ‘Nguzo Mama, Ngozi, Machozi ya Mwanamke), Falsafa ya Maisha
(mfano, ‘Kinjeketile, Kwenya Ukingo wa Thim) na Uchawi, Uganga na Itikadi
za Jadi (mfano, ‘Njia panda (muhanika), Ngoma ya Ngw’anamalundi,
Kinjeketile na Mafarakano).

NANI MUASISI WA KUTUMIA KANUNI ZA KI - AFRIKA KATIKA


TAMTHIL;IYA YA KISWAHILI?

Hoja hii ya nani mwanzilishi wa fasihi ya kiswahili ya kimajaribio katika


uwanja wa tamthiliya ilianza kujitokeza katika miaka ya 1980 ki mabishano.
Wahakiki wa mwanzo kabisa katika fasihi ya kiswahili kama wakina Nkwera
walianza kuizungumzia hoja hii mwishoni mwa miaka ya 1970 pasipo
mabishano.
Miaka ya 1980 na kuendelea ilikuwa ni miaka iliyowapambanisha mafahari
wawili katika uandishi wa tamthiliya ya kiswahili, Ebrahim Hussein na Penina
Muhando walitawala fikra, majukwaa, mijadala na makabrasha ya wahakiki wa
kazi za kifasihi.

Baadhi ya mawazo ya wahakiki nguli juu ya“nani muasisi katika matumizi ya


kanuni za ki-afrika katika tamthiliya ya Kiswahili?”
Nkwera (1977), anachambua kazi mbalimbali za Ebrahim Hussein na Penina
Muhando. Katika kujadili maendelao ya kazi za sanaa za Ebrahim Hussein,
muhakiki huyu anamtaja Bretch, mwandishi hodari na wa pekee wa michezo ya
kuigiza ya kimashariki. Nkwera anaanza kwa kusema:

“Hapo mwanzo Ebrahim Hussein aliathiriwa sana na Bretch katika utunzi wake.
Lakini kadri alivyoendelea kustawi katika uandishi wake wa sanaa za
maonyesho Ebrahim Hussein alianza taratibu kuchanganya jadi za kiafrika kama
vile masimulizi, utambaji, mianzo pamoja na miisho ya kifomula katika uandishi
wake. Hivyo Hussein ndiye mwandishi wa mwanzo kabisa aliyeanza kuzikiuka
taratibu za kiuandishi katika tamthiliya zilizofuata kanuni za ki-aristotle kwa
kuingiza ujadi wa ki-afrika katika kazi zake”.

Mhakiki huyu anahitimisha hoja yake hii kwa kujenga mazingira


yanayoonyesha kuwa mwanzilishi wa fasihi ya kiswahili ya kimajaribio katika
tanzu ya tamthiliya ya kiswahili ni Ebrahim Hussein, kwani ndiye mwandishi
wa mwanzo kabisa aliyeanza kuzikiuka taratibu za kiuandishi katika tamthiliya
zilizofuata kanuni za ki-aristotle. Nkwera ana hitimisha kwa kuchambua
tamthiliya ya Mashetani ya Ebrahimu Hussein na Pambo ya Penina Muhando.
Nkwera anasema:

“Pambo ni mchezo wa hali ya juu kimuundo. Hapana shaka yo yote kwamba


Penina Mlama (hapo awali alijulikana kwa jina la Penina Muhando)
ameathiriwa na Ebrahim Hussein kama Ebrahim Hussein alivyoathiriwa sana na
Bretcht, mwandishi hodari na wa pekee wa michezo ya kuigiza ya Kimashariki.
Nkwera anasisitiza kuwa kwa mtu aliyesoma Mashetani (OUP) hatasita kusema
kuwa Mama Mlama kaathiriwa na Ebrahim Hussein katika uandishi wake.
Jambo hili liwe ni kweli ama sivyo, Si jambo la msingi bali la maana zaidi
nikufahamu tu kwamba waandishi hawa wawili wamejitokeza kuwa mafundi na
mabingwa wa kuandika michezo ya kuigiza katika fasihi ya Kiswahili na ile ya
kimajaribio”.

King’ei (1987), anamtaja Ebrahim Hussein kama mwandishi wa sanaa ya


maigizo aliyefanikiwa katika kuchanganya mbinu za masimulizi ya mapokeo ya
fasihi simulizi kama vile ngano na vitendawili, na ufundi wa fasihi andishi
ambao ameutumia kutungia hadithi hizi kwa muundo wa maigizo jukwaani.
King’ei anaitaja tamthiliya ya Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi ya Ebrahim
Hussein kuwa mfano wa tamthiliya iliyoathiriwa sana na kumbo ya fasihi
simulizi.

Wafula (1999), anautaja mwaka 1971 kuwa ni mwaka wa mabadiliko makubwa


katika tasnia ya tamthiliya ya Kiswahili. Mhakiki huyu anamtaja E. N. Hussein
na tamthiliya yake ya Mashetani, kuwa ni moja kati ya tamthiliya za mwanzo
kabisa katika harakati za utumiaji wa kanuni za kijadi ndani ya kazi za kifasihi.
Wafura anasema:

“Hussein alijitokeza tena uwanjani, akathibitisha ameidhibiti bahari ya


tamthiliya kwa kutoa Mashetani. Tamthiliya ya Mashetani iliweka tarehe mpya
katika utungaji wa mchezo wa kuigiza katika lugha ya Kiswahili. Tamthiliya hii
ilionyesha kwa mafanikio makubwa, jinsi mapokeo ya kiafrika yanavyoweza
kutumika pamoja na mbinu za kisasa kufanikisha malengo ya kijukwaa”.

Katika kutafuta udhibitisho kwa waandishi wenyewe wanaozungumziwa


mvutano huu, utafiti huu ulifanya mahojiano na mama Penina Muhando kutaka
kujua mambo kadhaa juu ya suala hili. Mwanafasihi huyu mashuhuri
alilizungumzia suala hili kwa ufupi sana. Mama Muhando alisema:

“Vuguvugu la mabadiliko nchini Tanzania lilianza mwishoni mwa miaka ya


1970, katika kipindi hiki wasomi wengi wa kiafrika walianza kupinga taratibu za
kimaisha zenye umagharibi (taratibu za watu wa Ulaya). Wasomi hawa waliutaja
waziwazi ukoloni kama sababu kubwa iliyopelekea kuharibika kwa utamaduni
wa kiafrika. Baadhi ya waafrika walianza kubadili majina yao yenye asili ya
ukristo ama uislamu kwenda. Kipindi hicho tukiwa wasomi na wanaharakati
vijana tuliadhimia kuleta mabadiliko kwenye sanaa ya kiafrika kwa kuzitumia
kanuni za kiafrika hasa katika sanaa za maonyesho, ndipo sasa kanuni za jadi ya
ki-afrika kama masimulizi, utambaji, mianzo na miisho ya kifomula zilianza
kutumiwa na waaandishi. Ukweli ni kwamba katika kipindi hiki cha vuguvugu
la mabadiliko Ebrahim Hussein alikuwa tayari ameanza kuugua maradhi
yanayomsumbua hadi sasa, hivyo hakushiriki sana katika vuguvugu la
mabadiliko haya”.

Muhando (2013);

“Mimi na wasanii wenzangu kipindi hicho tulitunga michezo mingi na kwenda


kuicheza katika maeneo mbalimbali “live”, tuliandika michezo mingi sana
yenye kanuni za kijadi na mingi kati ya michezo hiyo haijachapishwa na
kwasababu kilikuwa ni kikundi michezo mingine sijui hata ilipo. Na
unapozungumzia mageuzi ama mabadiliko katika tasnia hii ya sanaa za
maonyesho usitazame kazi zilizoandikwa tu vitabuni na kuwekwa ujadi ndani
yake, lengo la mabadiliko yetu kipindi hicho ni kuhakikisha kuwa sanaa za
jukwaani zinaigizwa katika maeneo husika ya wanajamii na kuleta mwamko wa
kimaendeleo zinakuwa na nguvu kuliko zile zinazoandikwa na kuishia kwenye
vitabuni tu”.

Maelezo ya Muhando yanaonyesha mwelekeo kuwa yeye pamoja na wasanii


wenzake kipindi hicho ndio walikuwa waanzilishi wa kutumia kanuni za jadi ya
ki-afrika katika tamthiliya za kiswahili.
(Williady, 2013) katika Utafiti wake, anaunga mkono mawazo ya Nkwera
(1977), King’ei (1987), Wafula (1999), Sengo (1977), yanayodai kuwa mwasisi
wa kutumia kanuni hizi katika tamthiliya za Kiswahili ni Ebrahim Hussein.
Uungaji mkono huu umetokana na sababu moja kubwa. Mwaka 1971, Ebrahim
Hussein alichapisha tamthiliya yake inayoitwa Mashetani, kama wasemavyo
wahahiki kuwa Mchezo huu wa Mashetani umekaa kishetani shetani ili msomaji
au mtazamaji auelewe vizuri inampasa ajigeuze shetani katika ulimwengu wa
chukulizi za kifasihi, ndipo atapata kuuelewa. Mwaka 1975, takribani miaka 4
baadaye tangu kuchapishwa kwa mchezo wa Mashetani, Penina Muhando
alichapisha tamthiliya yake inayoitwa Pambo, ama hakika Pambo ni mchezo wa
kiwendawazimu wendawazimu, ili msomaji auwelewe vizuri inampasa kujitia
katika wendawazimu wa kifasihi. Hakuna tofauti kubwa kati ya michezo hii
miwili ya Mashetani na Pambo, inaonekana Penina Muhando alichota baadhi ya
misingi ya Hussein katika uandishi wake. Haitoshi, mwaka 1976, Ebrahim
Hussein alichapisha michezo yake miwili aliyoiweka katika kijitabu kimoja,
Jogoo kijijini na Ngao ya jadi. Michezo hii imeandikwa kwa utaratibu wa fasihi
simulizi, kuna ngano, watambaji, hadhira na kuna kuanza na kukamilisha kazi
ya fasihi kikanuni (mianzo na miisho ya kifomula). Mwaka (1984), miaka
takribani nane (8) baadaye Penina Muhando alichapisha tamthiliya yake
inayoitwa Lina Ubani, tamhiliya hii inaonekana kuwa na sifa sawa na zile za
Jogoo kijijini na Ngao ya jadi. Kwa hoja hii utafiti huu unaunga mkono mawazo
ya Nkwera na wenzake kuwa mwasisi wa michezo yenye kukiuka taratibu za ki-
aristotle na kufuata taratibu za jadi ya ki-afrika ni Ebrahim Hussin. Kauli hii ya
kumtaja Ebrahim Hussein kuwa ndiye mwasisi wa tamthiliya hizi za kimajaribio
haitoi ukweli kuwa Penina Muhando naye anaumuhimu mkubwa sana katika
tamthiliya ya Kiswahili.

Nadharia
NADHARIA HUTUMIWA SANA KATIKA UTAFITI

HUWEZI KUFANYA UTAFITI BILA NADHARIA

KARIBU KWENYE DARASA LA NADHARIA ZA KISWAHILI

MAANA YA NADHARIA

(Williady, 2013), Nadharia ni maelezo yakinifu kuhusu kitu, tajiriba, mahalifa


au upumbavu na mafanikio au maangamizi yanayochomoza katika jamii. Hivyo
nadharia hufungamana na mambo mbalimbali ya jamii kama vile mbinu,
maarifa, tasinifu, mikabala na mienendo mbalimbali ya jamii.

1. NADHARIA YA UPOKEZI (MWITIKO WA MSOMAJI)

Nadharia ya Upokezi (mwitiko wa msomaji) ambayo husisitiza nguvu ya


msomaji. Nadharia ya Upokezi (Reception Theory) iliasisiwa na wahakiki wa
waasisi wa Kijerumani mwishoni mwa miaka ya 1960.Miongoni mwa waasisi
wa nadharia hii ni Robert C. Holub,Hans Robert Jauss na Wolfagang
Isser.Katika kitabu chake Reception Theory (1984), Holub anaelezea nadharia
ya Upokezi kuwa ni Mabadiko ya jumla ya umakinikiaji kutoka kwa mwandishi
na kazi yake kwenda kwa matini na msomaji”
Nadharia ya upokezi inaakisi mabadiliko ya mbinu katika historia ya fasihi na
ilizingatiwa kama jibu kwa jamii,wanazuoni na maendeleo ya fasihi huko
Uerumani Magharibi mwishoni mwa miaka ya 1960.Kwa mujibu wa Holub,
nadharia ya Upokezi ulikuwa ni njia ya Kimapnduzi kwa wahakiki wa kisasa.

Waitifaki wa nadharia hii wanashiilia msimamo kuwa kazi ya fasihi hupata


maana baada ya matini na msomaji kuadhiriana.Msomaji au mpokeaji ndiye
huipa maana kazi ya fasih.

Kwani huiona na kuilinganisha na uzoefu wake wa maisha. Kielelezo hiki kipya


cha uhakiki hutilia maanani dhima ya msomaji.Hans Robert Jauss katika makala
yake “The change in the Paradigm of Literary Scholarship” (1926) ambaye
anachukuliwa kama mmoja wa mihimili ya nadharia hii ya Upokezi anaelezea
umuhimu wa kuielezea kazi ya Fasihi.Isser anaiona kazi ya Fasihi kama kitu au
tukio lililo nje ya muktadha na historia.

Anasema kuwa ili kazi ya fasihi ieleweke ni lazima ushiriki wa msomaji uoane
au upatane na maana inayojitokeza katika kazi ya Fasihi.

Kwa hiyo basi , nadharia ya Upokezi hufasili Fasihi kama mchakato wa namna
msomaji na wanavyoathiriana.Uzoefu wa maisha wa msomaji unaweza kutoa
tafsiri tofauti kwa kazi ya fasihi kutoka msomaji mmoja na mwingine.

2.NADHARIA YA ONTOLOJIA YA KIBANTU.


Nadharia ya Ontolojia ya Kibantu. Kuna wataalamu mbalimbali
waliozungumzia nadharia hii. Kwa jumla, wataalamu hawa wameeleza maana
ya Ontolojia kuwa ni mtazamo unaohusu kuwepo kwa kitu katika dunia na
kuangalia vitu katika uhasilia wake (Nicholaus 2011).

Ontolojia inaweza kutazamwa kwa namna tatu: kama taaluma, kama falsafa na
kama nadharia. Hivyo kwa kuwa utafiti huu ulichunguza “Mabadiliko ya
kiuandishi kutoka kanuni za Ki-Aristotle kwenda kanuni za jadi ya Ki-Afrika”,
kipengele cha Ontolojia ya Kibantu kinachoweza kutumika katika kazi za fasihi,
tuliona ni vyema kutumia Ontolojia kama nadharia katika utafiti huu, kwani
imewezesha utafiti huu kufikia malengo yake, pia ilihusiana na mada
iliyoshugulikiwa.

Kimsingi kuna mitazamo minne kuhusu Ontolojia ya Kibantu. Mitazamo hiyo


ni, ule wa falsafa ya kisiasa (Itikadi ya kisiasa), mtazamo au falsafa ya
Kihikimati (Sagacty), wanafalsafa waliojikita katika kurekodi imani katika
utamaduni wa mwafrika (Ethnofilosofia), na falsafa ya Kiuweledi.

Wanaitikadi wa kisiasa walichunguza masuala ya undugu wa kifamilia, ujamaa


na kujitegemea ndani ya Afrika. Wanasiasa hao ni Julius Nyerere, Leopold
Senghor na Kwame Nkurumah. Lengo lao lilikuwa ni kutaka kutafuta uhuru wa
kweli kwa waafrika ili kurudisha heshima kwa mwafrika kama ingewezekana.

Mtazamo wa Kihikimati umejikita katika masuala ya uhuru, hekima na desturi


za watu. Waanzilishi wa mtazamo huu wameshawishika kwamba falsafa ya
kiafrika haiangalii vitu vyote vinavyohusu kazi. Lengo lao walitaka kuonesha
kwamba ujinga sio hali ya kifalsafa na ujinga upo kwa kila jamii, ujinga wa
mwenzako waweza kuwa uhuru kwake. Waanzilishi wa falsafa hii ni Odera H.
Oruka na Marcel Griaule’s.Marcel Griaule’s alifanya mazungumzo na
Oyotemmeli kiongozi wa kabila la Wadogoni na matokeo yake walipata falsafa
ya kidini ya wadogoni.
Ethnofilosofia hujishughulisha na ukusanyaji wa mitazamo ya kiulimwengu
kutoka katika tamaduni mbalimbali za waafrika. Hii imejikita katika masuala ya
imani, masimulizi na misemo ya watu. Muunganiko huo umeunganishwa na
Paulin Hountondji. Wengine waliojihusisha na falsafa ya kiafrika katika
mtazamo huu ni Placid Tempels, Leopald Senghor, John Mbiti na Alex Kagame.
Hivyo, mtazamo huu umejikita zaidi katika masuala ya mila, desturi na imani za
jamii.

Falsafa ya Kiuweledi imejikita katika uchambuzi na ufafanuzi wa ukweli. Zaidi


inajihusisha na uhakiki, na hoja ndizo sifa za msingi kwao. Waanzilishi wa
falsafa hii ni Paulina Hountondji, Kwasi Waredu, Odera Oruka na Peter
Bodunrin. Wanasema kuwa falsafa ya kibantu kwa sasa inaitwa Metafilosofia,
na imejikita katika kuangalia maudhui ya msingi. Wao wanahoji kwamba falsafa
ya Afrika ni ipi?

Roberto (1996) anasema Ontolojiani nadharia inayohusu kuwapo, yaani ni


nadharia inayoangalia yaliyokuwepo na yale ambayo hayakuwepo, halisi na
yasiyo halisi, tegemezi na vinavyojitegemea.

Parrinder (1969) anasema kuwa nadharia ya kibantu inahusisha mwafrika na


imani yake. Hujumuisha maisha, mazingira pamoja na fikra zake. Pia anasema
kuwa mawazo ya mwafrika hujengwa katika misingi ya nguvu mbalimbali
ambazoni Mungu, binadamu, wanyama, mimea na kadhalika.

Wataalamu wengine waliozungumzia nadharia ya Ontolojioa ni: Husserl (1913),


Tugendhat (1928), Wolff (1928), Gruber’s (1993), Bolzano (1996), Guariono
(1998), Wamitila (2008) na Cocchiarella (2007).

Kwa jumla, wataalamu hawa wameeleza mengi juu ya nadharia hii, jambo
lililosisitizwa sanana wataalamu wengi waliojadili nadharia hii ni kuhusu
uchaguzi wa Ontolojia nzuri na namna ya kutumia nadharia hii. Wanasema
Ontolojia nzuri ni ile inayohusisha njia za Kisayansi na kutupatia njia chache na
rahisi ambazo zitaelezea mambo mbalimbali katika ulimwengu. Pia nadharia hii
inatukuza sana Ubantu na kumuona mwafrika kama kiumbe bora mwenye
uwezo wa kubuni na kusimamia mambo yake kwa usahihi. Mbali na kutumia
Ubantu (U-Afrika), nadharia hii inaeleza mambo kadhaa ambayo ni sehemu ya
ufahari kwa waafrika, mambo hayo ni pamoja na dhana ya familia pana,
kuamini uzazi kuwa ndio njia ya uzima wa milele, yenye kuhashiria umuhimu
wa binadamu, na Ugumba ni laana na utupu kwa binadamu, kuabudu katika
Mungu na miungu na kuheshimu Wahenga. Pia huhusisha na imani kuhusu
uchawi, na sihiri, na ndani yake kuna masuala ya uganga. Pia umri kwa waafrika
una nafasi kubwa sana katika jamii na unabeba hekima za mtu.

3.UJUMI (AESTHETICS)

Ujumi ni nini?

Ujumi ni tawi la falsafa linaloshughulika na uzuri, ubaya, ladha, n.k.

AU

Ujumi ni elimu ya sheria na kanuni za sanaa.


Neno ujumi kwa kiingereza linajulikana kama “Aesthetics”. Neno hili
limetoholewa kutoka katika lugha ya kigiriki “Ais - thesis”, likiwa na maana ya
“Hisia” (Feelings), hasa hisia za akilini (Mental perception).

Alexander Gottlieb Baumgarten (mjerumani) ni miongoni mwa wanafalsafa


yalioshungulikia kwa kina juu ya falsafa hii ya Ujumi. Baumgarten alidokoa
baadhi ya mawazo fasaha kutoka kwa Leibniz. Leibniz alizungumzia mambo
makubwa mawili amabayo ni LOGOS na ETHOS.

LOGOS, ni mantiki itokanayo na neno la maharifa au sababu ipelekeayo


uwelewa mpya au kuyachekecha mawazo makuukuu na kupata neno lenye
kuchukua mkondo mpya.

ETHOS, ni desturi ama mguso, tabia ama kaida Fulani ndani ya jamii ambazo
hufanya matakwa yahusuyo jamii Fulani tu.

Baumgarten, alikiendeleza kipengele cha mguso na hisia na neno “Aesthetics”


likaanzishwa.

Kabla falsafa mpya ya Aesthetics haijachukua kasi yake, hapo awali masuala ya
hisia yaliwekwa chini ya nadharia ya hisia za akili (mental perception). Dhana
ya ujumi ilitoka kwenye nadharia ya hisia za akili katika karne ya 18 na
kuitwa “Falsafa ya uzuri” au “Falsafa ya sanaa” au yote mawili kwa pamoja.
Baadaye ujumi uliachana na falsafa na kuwa tawi linalojitegemea la elimu.

Kabla ya Baumgarten, ushairi na sanaa kwa ujumla ilijadiliwa kitaalamu katika


kapumoja. Hii inamaana kwamba ushairi haukutofautishwa na muziki au
uchoraji ama ususi, vyote vilielezwa kwa pamoja.
Baumgarten akaigawa dhana hii katika maeneo mawili ambayo ni uzuri na
sanaa.

1. UZURI (The good or the truth).

Uzuri ni ukamilifu wa hisia za akili unaoleta kulitazama jambo au mambo


Fulani katika mtazamo chanya, haijalishi, kwani mwingine anaweza
kulichukulia jambo hilo kimtazamo hasi lakini mtazamo wake hauondoi uzuri
wa chanya kwa atazamaye chanya.

2. SANAA

Sanaa ni ufundi wa kuunda jambo. Twaweza kuueleza uzuri kupitia sanaa. Sanaa
yaweza kuupambanua uzuri kwa viwango vya juu zaidi kuliko jambo lolote lile.

Tafadhali wasiliana na mwl. Majumbeni kwa,

0762 – 957493

0768 – 625660

hwilliady@ymail.com
majumbeni@gmail.com

4. NADHARIA YA UFEMINISTI ( Mtazamo wa kike)

(Williady, 2015) Nadharia hii inahistoria ndefu duniani, ikimaanisha ni moja ya


nadharia zilizopata kutokea miongo mingi iliyopita. chanzo cha kuibuka kwa
nadharia hii ni vuguvugu la kutaka kufuta kabisa uonevu wa mwanaume kwa
mwanamk. nadharia hii inadai kuwa chimbuko la uonevu na ukandamizaji
unaofanywa na wanaume kwa wanawake ni uroho wa mwanaume katika
kumtawala mwanamke. Kwaufupi, ajaenda kuu ya ufeministi na mafeministi ni
kumaliza kabisa utawala wa mwanaume kwa mwanamke.

moja ya wadau waliochangia sana kuendelea kwa nadharia hii kwa kasi ni
Adrew Dworkin. Mwaka 1976, akiwa katika mji mkuu wa Uingereza, London,
alitoa mapendekezo makali katika kukomesha utawala wa mwanaume kwa
mwanamke, Dworkin anasema: Ili kufanikisha, tunahitaji kubomoa kabisa
muundo wa mihimili ya utamaduni wa jamii kama vile sanaa, kanisa, sheria,
kaya zinazodhibitiwa na baba, jamii na taswira zote za asasi, mila, desturi
ambazo zinamwona mwanamke kuwa mtu ovyo.

WATAALAMU MBALIMBALI WALIVYOZUNGUMZIA MAANA YA


UFEMINISTI

Nadharia ya Ufeministi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kama vile:


Wamitila (2003:253), hii ni nadharia ambayo imewekewa msingi na msukumo
mkubwa pamoja na nia ya kupigania ukombozi wa mwanamke kutokana na
pingu za kiutamaduni, kidini, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Hii ni nadharia
ambayo inasaili na kudadisi itikadi ya kiume ambayo imekuwepo katika jamii
kwa kipindi kirefu. Kudadisi pia fasiri za kiume za fasihi pamoja na mikabala ya
kiubabedume.

Ntarangwi (2004:45), ni nadharia ambayo inajaribu kukiuka mitazamo ya kiume


ambayo yaelekea inatumiwa sana katika jamii.

Mukobwa M. nadharia ya ufeministi imetokana na mkondo na harakati za


kutetea haki za wanawake ulimwenguni na imejikita katika imani ya usawa wa
kijinsia, kijamii, kisiasa na kiuchumi.

(Williady, 2015) Ninadharia iliyojaribu kuvunja mwiko wa mfumo dume hapa


dunia kwa kuanzisha mapambano ya usawa wa kijinsia, bilashaka majaribio
haya bado hayajafanikiwa.

Kwa jumla, nadharia ya ufeministi ni nadharia iliyojikita katika kupinga


ukandamizaji wa mwanamke katika jamii hususan katika nyanja za kisiasa,
kiuchumi, na kiutamaduni.

KUIBUKA KWA UFEMINISTI NA HARAKATI ZA KUIENDELEZA


NADHARIA HII

Uhakiki wa kifeministi ulishika kasi miaka ya 1960 na kuendelea kukua na


kuishia kuwa muhimu katika miaka ya hivi karibuni. Zipo kazi kadhaa
zilizoandikwa kabla na kulimulika suala hili kwa namna moja ama nyingine.
Kazi kuu mbili zinazorejelewa hapa ni A Room of One’s Own ya Virginia Woolf
na A virdiction of the Right of women ya Mery Wollsto Necraft.
Hata hivyo, kazi iliyoishia kuwa na mchango mkubwa katika kuuweka msingi
wa uhakiki wa ufeministi ni kazi maarufu ya mwandishi wa Kifaransa, Simone
de Beauvoir iitwayo, The Second sex, 1952 katika kitabu hiki, mwandishi huyu
anachukuwa mkabala wa kiharakati kwa kushambulia na kukosoa baadhi ya
asasi zinazochangia katika kumdhalilisha au kumdunisha mwanamke. Asasi kuu
anazozishambulia ni ndoa, dini na utamaduni.

Nadharia ya ufeministi ilichimbuka huko Marekani katika harakati za


kukomesha biashara ya utumwa mwaka 1830. Wanawake wakaanzisha harakati
za kupigania haki za mwanamke.

Wamitila (2006:160-161) na Ntarangwi (2004:52-56) wamebainisha malengo


mbalimbali ya ufeministi.

Ni kweli kwamba kuna baadhi ya malengo ya ufeministi yanakinzana na maisha


halisi ya mwanamke wa Kiafrika lakini baadhi ya malengo hayo yanasawiri
maisha halisi ya mwanamke wa kiafrika kama ifuatavyo:

Kubainisha umuhimu wa mwanamke, kutokana na mwanamke kukulia katika


jamii zenye mfumodume. Umuhimu wake haukuonekana, ndiyo maana
ikaanzishwa nadharia ya ufeministi ambayo yenyewe iligundua umuhimu wa
mwanamke katika jamii. Umuhimu wake upo katika Nyanja zote za kiuchumi,
kijamii, kisiasa na kiutamaduni. Mfano, katika nyanja ya kisiasa mwanamke
anaweza kuwa kiongozi bora na mwenye ushauri. Hili linajidhihirisha katika
riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ (1994).
Mwandishi anathibitisha hili anaposema:

“Tunayo karibu miaka ishirini ya uhuru! Lini tutampata mwanamke wa kwanza


awe waziri atakaye husishwa na maamuzi yatakayoongoza nchi yetu huko
tuendako? Kumbe nguvu walizonazo wakina mama, uwezo wao wa kupambana,
na kujihusisha kwao bila kutegemea kupata faida yoyote ni mambo ambayo
hayahitaji tena kuthibitishwa. Wanawake wamewainua wanaume wengi kwenye
ngazi za juu.” (uk.82)

Katika nyanja ya kijamii, mwanamke ni mlezi wa familia. Mfano, Ramatulayi


anailea familia yake kwani ameweza kulipa bili ya maji, umeme bila hata
kumtegemea mwanaume. Mfano, mwandishi anasema:

“Licha ya mzigo niliokuwa nao tangu zamani, nikaubeba na ule uliokuwa wa


Modu. Ununuzi wa vyakula muhimu ulinishughulisha kila mwisho wa mwezi.
Nilihakikisha kwamba sikuwa na upungufu wa nyanya au mafuta, viazi
mviringo na vitunguu wakati ambapo vyakula hivi viliadimika sokoni…
Nilikuwa mwangalifu kuzilipa bili za maji na umeme pindi zilipofika.” (uk.69)

Lengo hili la ufeministi linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika,


kwa kuwa mwanamke wa Kiafrika anaonekana hana umuhimu katika jamii, pia
anaonekana kuwa dhaifu ambaye hawezi kuiendesha familia yake bila msaada
wa mwanaume hii ni kutokana na jamii nyingi kuendeshwa na mfumodume.

Kuorodhesha kuwa kihistoria wanawake wamekuwa ni tegemezi na wasaidizi


wa wanaume, ni kweli kihistoria wanawake wamekuwa wategemezi na
wasaidizi wa wanaume. Mfano katika tamthiliya ya Nguzo Mama iliyoandikwa
na Penina Muhando (2007) tunaona mhusika BI MOJA alivyokuwa
akimtegemea mume wake na kutaka anunuliwe kanga. Mwandishi anasema:

“BI MOJA: (kwa Shaabani): Kama ulijua kufika sasa hivi nipe hela ya kanga
bwana meli meli hii hainikosi leo utanipa hela hizo kanga nikakate. Mwezi wa
tatu huu kanga sizijui.

Shaabani: Nimekuambia mimi hela sina. Sasa unataka nikaibe?”(uk.31-


32)

Ni kweli kwamba mwanamke wa kiafrika amekuwa tegemezi katika jamii,


kwani humtegemea mwanaume katika mambo mbalimbali ya kifamilia. Kwa
mfano kutafuta au kununua mahitaji ya nyumbani kama vile chakula, mavazi
yake na watoto wake au kulea watoto wake.

Kuondoa ukandamizaji wa mwanamke kutokana na pingu za kiutamaduni,


kijamii, kidini, kisiasa na kiuchumi. Jamii nyingi za Kiafrika zimejengeka katika
mfumodume, hivyo basi jamii zinamkandamiza mwanamke kutokana na pingu
hizo. Katika kulithibitisha hili waandishi wa kazi za fasihi nao hawakuwa
nyuma kulizungumzia katika kazi zao na lengo ni kuondoa mfumodume
uliojengeka muda mrefu katika jamii.

Kwa upande wa kiutamaduni mwanamke ameonekana kukandamizwa kwa


kuonekana hana mamlaka hata ya kurithi mali za mumewe au zake mwenyewe,
badala yake hata akifiwa na mumuwe anapigwa, anafukuzwa na kudhalilishwa.
Penina Muhando anayathibitisha haya katika tamthiliya yake ya Nguzo Mama
kwa kumtumia BI SABA pale anaposema:

“Akalia Bi Saba tena akalia

Hana wa kumsaidia

Mumewe kafa nduguze wakaja juu

Pesa wamechukua senti tano haikubaki

Vyombo na nguo zote wakagawana

Roho ilimpasuka Bi Saba kuwaona hao ndugu

Walivyogombania mali wasiyoichuma…

Sasa juu ya yote haya wamerudi kufagia

Hata ufagio wamebeba

Na lawama kumtupia eti pesa kazificha.” (uk.39)

Pia mwanamke anaonekana anajishughulisha na kazi mbalimbali za kujiletea


maendeleo yake binafsi lakini anarudishwa nyuma kwa kukandamizwa na
mwanaume. Penina Muhando anayathibitisha haya kwa kumtumia BI PILI
ambaye alikuwa anapika pombe ili kujikwamua katika hali ngumu ya maisha
lakini mumewe SUDI alizichukua hela zote alizokuwa alizozipata. Kwa mfano,
mwandishi anasema:

“BI MSIMULIZI: Upishi wa pombe balaa ulimzushia

Visa na mikasa Bi pili havikumuishia

Pesa alizipata kutokana na hiyo pombe

Lakini visa vya pombe hiyo pesa hazikufidia”

SUDI: (kwa Bi Pili) Nani kalewa? Umeninywesha wewe?

Wee!hawara zako ndiyo wamekutia jeuri unaninyima pesa.

Toa pesa sasa hivi (Anampiga) Bi Pili anakimbia huku


akilia.” (uk.16)

Vilevile, mwanamke alikuwa anakandamizwa kwa kulazimishwa kurithiwa na


kaka au ndugu wa mume pindi anapofiwa na mumewe. Mwandishi
analithibitisha hili katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii pale anaposema:

“Tamsiri, zitapike hizo ndoto zako za kutaka kuniposa.

Umeshakaa nazo kwa siku arobaini. Kamwe sitokuwa mkeo.”(uk.81)

Kwa upande wa kisiasa, mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa kuonekana


hawezi kuwa kiongozi bora wa kuiongoza nchi ndio maana hata nafasi za
wanawake zilikuwa chache huko bungeni. Katika riwaya ya Barua Ndefu Kama
Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ mwandishi anayadhihirisha haya kwa
kumtumia Ramatoulayi ambaye akilalamika kuhusu ukandamizwaji wa
wanawake huko bungeni pale anaposema:

“Wanawake wanne, Dauda, wanne miongoni mwa wabunge mia moja uwiano
gani huu wa kimzaha! Wala hakuna uwakilishaji wa kimkoa” (uk.81)
Kwa upande wa kijamii, mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa kupigwa na
mumewe bila sababu zozote za msingi. Hili linajidhihirisha katika riwaya ya
Rosa Mistika iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi (1988) kwa kumtumia
mhusika Zakaria ambaye alikuwa anampiga mkewe bila sababu. Mwandishi
anasema:

“Regina tangu aolewe hakuwa na raha! Alikuwa akisumbuliwa na kuteswa na


mumewe kwa kosa lisilokuwa lake. Katika kijiji chote cha Namagondo
hapakuwa na mwanamke aliyekuwa akipigwa karibu kila juma kama Regina.
Wanawake wengi kijijini walijiuliza kwa nini hakutaka kumuacha bwana wake.
wengine walimuonea huruma, wengi lakini walimuona mjinga.” (uk.3)

Pi, mwanamke alikuwa anakandamizwa kwa kuonekana kuwa yeye ndiye


mwenye majukumu ya malezi, kwa hiyo hata watoto wakiharibika
anayelaumiwa ni mwanamke. Euphrase Kezilahabi analithibitisha hilo pale
anaposema:

“Lete hiyo barua iko wapi? Pamoja na shilingi ulizopewa unafikiri sisi hapa
maskini. Rosa alipigwa tena na tena. Makofi yalikwenda mfululizo hata damu
zikamtoka puani na mdomoni. Baba nihurumie sitarudia tena… Zakaria
hakujali alichukua fimbo na kuongozana na bintiye mpaka chumba cha watoto
hali akinguluma lazima unioneshe barua hiyo unataka kuniletea umalaya wa
mama yako hapa.” (Uk.7)

Vilevile, mtoto wa kike alikuwa anaonekana hana thamani katika jamii, na


watoto wa kiume ndio waliopewa kipaumbele. Euphrase Kezilahabi
anathibitisha haya katika riwaya ya Rosa Mistika kwa kumtumia Zakaria
ambaye kabla ya kumpata mtoto wa kiume alikuwa anamnyanyasa sana mke
wake lakini baada ya kujifungua mtoto wa kiume manyanyaso yaliisha na
alimpenda sana mkewe. Mwandishi anasema:
“Zakaria alirudi nyumbani siku hiyo. Alikuwa amekwisha pata habari hizo
njiani. Alimbeba mtoto. Alimpa pongezi mke wake. Regina sasa mji huu
umekuwa wako. Asante Regina alijibu akitabasamu, alijiona anauwezo wa
kuzungumza.” (uk.24)

Lengo hili linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwani


mwanamke hatakiwi kurithi mali yoyote pindi wazazi wake wanapofariki au
mumewe anapofariki. Pia mwanamke kushindwa kupewa nafasi ya kutoa
maamuzi yoyote katika masuala ya kiukoo. Kwa upande wa dini mwanamke
anakandamizwa na kuonekana dhaifu hivyo kutokuwa na nafasi ya kuongoza
waamini. Mfano, dini ya Kiislamu na baadhi ya madhehebu ya Kikristo.

Lengo lingine ni kuzitambua na kuzibainisha dhamira kuu katika kazi


zilizoandikwa na wanawake. Dhamira kuu ni dhamira inayomsukuma
mwandishi katika kuandika kazi ya fasihi. Baadhi ya waandishi wanawake
wameonesha dhamira kuu katika kazi zao kama ifuatavyo:

Nguzo Mama iliyoandikwa na Penina Muhando (2007) imebeba dhamira kuu


ambayo ni ukombozi wa mwanamke. Ukombozi huo upo katika nyanja
mbalimbali kama vile kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa. Mfano,
mwandishi ameonesha wanawake wanavyojishughulisha katika kuinua uchumi
wao, kwani walikuwa wakiuza vitambaa na kupika pombe. Mwandishi
anathibitisha haya kwa kusema:

“BI TANO: Yaani mnasema mimi mvivu siyo nimezunguka mji mzima na zigo
hilo halafu mnaniambia mimi mvivu. Nawaambia watu hawataki kununua au
mnataka niwagawie bure.”

BI NANE: Lakini kwa nini wakatae kununua hivi, mbona vile vya mwanzo
walivinunua? (uk.16).

Vilevile, Katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ


(1994) suala la ukombozi wa mwanamke limejitokeza kama dhamira kuu.
Ukombozi huu umejikita katika nyanja za kisiasa, kiutamaduni, kijamii na
kiuchumi.

Mfano, katika nyanja ya kijamii, mwandishi ameonesha jinsi ya kumkomboa


mwanamke kielimu, pale anaposema:

“…Shangazi Nabu anampeleka Nabu mdogo katika shule ya Kifaransa huko.


Huko Nabu alijifunza aina mbalimbali za mapishi, matumizi ya pasi na zana za
kutumia na kumenyea...” (uk.39)

Lengo hili linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwa kuwa


tangu mwanzo wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuwa viongozi, badala yake
wanaume ndio waliochukuwa jukumu hilo la uongozi katika jamii. Pia,
wanawake hawakuruhusiwa kupata elimu wakitegemezwa katika majukumu ya
nyumbani na kuandaliwa kwenda kuolewa na kuja kuwa walezi wa familia.

Kuichunguza historia ya kifasihi ya jadi ya kike na kuwamulika waandishi wa


kike waliotambua hali za wanawake na ambao wanaweza kuchukuliwa kama
vielelezo kwa wasomaji wao. Hapo awali kazi mbalimbali za kifasihi za jadi za
kike zilielezwa na waandishi wa kiume. Lakini nadharia hii imemulika
waandishi wa kike wanaotambua hali mbalimbali na wameamua kuandika kazi
mbalimbali ambazo zinaelezea matatizo ya wanawake. Mfano, katika tamthiliya
ya Nguzo Mama mwandishi anaelezea jinsi wanawake wanavyonyanyaswa na
kuachiwa majukumu ya kulea familia, kuchukuliwa mali zilizoachwa na waume
zao baada ya kufariki. Mfano, mwandishi anasema:

“…Haa! Shemeji mmerudi kuchukua hata kitanda! Hata sufuria! Nitalala wapi
na nitapikia wapi jamani!” (uk.39)

SUDI: Haya nipe pesa ulizokwisha kupata.

BI PILI: Hee! Kwa nini nikupe?

SUDI: Leta pesa upesi kabla sijakukong’ota.” (uk.13)


Mariama Bâ naye ni kielelezo kwani ameelezea matatizo mbalimbali
yanayowakumba wanawake na namna wanavyokabiliana na matatizo hayo.
Mfano mwandishi anasema:

“… Ramatulayi, Acha nisikilize mimi zaidi; Redio ya Kankan ilinifahamisha


kwamba ulikataa kuolewa na Tamsiri. Ni kweli? Ndio.” (uk.87)

Mwandishi anaonesha jinsi mhusika Ramatulayi alivyojitambua na kukataa


kurithiwa na Tamsiri, pia anamkataa Dauda ambaye alitaka kumrithi baada ya
kufiwa na mume wake.

Kupitia lengo hili tunaona wanaufeministi wameongelea kuhusu wanawake tu


ambao ni vielelezo katika kazi za fasihi, lakini wapo wanaume ambao
wamezungumzia masuala mbalimbali yanayowahusu wanawake. Mfano,
Shaaban Robert aliyeandika Wasifu wa Siti Binti Saad.

Kudhihirisha kuwa kuna sifa fulani za kike na uzoefu fulani wa kike katika
uwazaji, hisia, kutathmini, kujiangalia na kuuangalia ulimwengu wao wa nje.
Uzoefu fulani wa kike unajitokeza katika uwazaji na jinsi wanavyousawiri
uhalisi. Kazi ambazo zinamsawiri mwanamke kwa njia chanya, mfano ni riwaya
ya Kiwasifu ya Shaaban Robert Wasifu wa Siti Binti Saad. Kuna mashairi
kadhaa aliyoyatunga mwandishi ambayo yanaendeleza suala hili la uchanya wa
wanawake katika jamii. Mfano wa usawiri wa wahusika linathibitishwa pale
mwandishi anaposema:

“Siti binti Saad,

Ulikuwa mtu lini,

Ulitoka shamba,

Na kaniki mbili chini,

Kama si sauti,

Ungekula nini?” (uk.22)


Hisia: mfano, katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii kupitia mhusika Daba
alivyomwambia mama yake kuhusu Benetuu. Mwandishi anasema:

“Hasira ya Daba iliongezeka zaidi jinsi alivyozidi kuichambua hali ilivyokuwa.


“Mama! Vunja ndoa yako! Achana naye mtu huyu hajatuheshimu, si wewe wala
si mimi… sitaki kukuona unagombania mwanaume na mwanamke mwenye umri
sawa na mimi.” (uk.52)

Lengo hili la wanaufeministi, linaendana na hali halisi ya wanawake wa


Kiafrika, kwa kuwa mawazo ya mwanamke jinsi anavyojiwazia yeye
mwenyewe au kuwawazia wanawake wenzake hutofautiana . vilevile, hisia za
mwanamke zinaweza kudhihirika katika maandishi na kuonesha jinsi
wanavyowaza katika hali ya kawaida.

HITIMISHO

Lengo la nadharia ya ufeministi lilikuwa ni kuondoa unyanyasaji wa kijinsia


hasa kwa mwanamke. Hivyo basi, malengo ya ufeministi yalijikita katika
kumnasua mwanamke kutoka katika pingu za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na
kijamii. Malengo haya ndiyo yanayoleta ukinzani wa maisha halisi ya
mwanamke wa Kiafrika. Hali hii imeleta mabadiliko katika maisha ya
wanawake wa kiafrika, kama vile kutaka haki ya elimu, kumiliki mali, kurithi
mali, kutaka nafasi za uongozi, pia kuwa na maamuzi ya kifamilia au kiukoo,
katika kupingana na pingu za maisha.

You might also like