You are on page 1of 1

Western Tanzania Conference P O BOX 519,

KIGOMA
of Seventh-day Adventists TANZANIA
SECRETARIAT ' +255 766 822 172
' +255 782 822 172
azzarachel@gmail.com

Alhamisi, Aprili 27, 2023

Mchungaji wa Mtaa
Mzee wa Kanisa
Karani wa Kanisa

Ndugu katika Kristo,

YAH: JUMA LA UREJESHAJI JUNI 10-17, 2023

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Jina la Mungu lipewe sifa.

Rejea kichwa hapo juu.

Kanisa la Waadventista Wasabato limeona vema kuwa na Juma la Urejeshaji duniani


kote. Kwa kushirikiana na Waadventista ulimwenguni mwote Western Tanzania
Conference itakuwa na Juma la Urejeshaji litakaloendeshwa katika kila Kanisa kama
ifuatavyo:

Tarehe: 10-17 Juni 2023


Fungu Kuu: Luka 1520
Mada Kuu: Huruma
Mhusika: Kila Baraza la Kanisa, Kila Kiongozi katika Kanisa, Kila Mshiriki
Kamati Itakayoratibu Juma Hili katika Kila Kanisa: Kamati ya Malezi na Urejeshaji
Mtoa Taarifa wakati wa Tukio (kwa Mchungaji na Conference): Karani wa Kanisa

Dhumuni la msingi la Juma hili ni kuwarudisha waliokuwa Waadventista Wasabato na


baadaye waliliacha Kanisa kwa sababu yoyote ile.

Kwa barua hii unaombwa tangu sasa umkumbuke kila aliyerudi nyuma na kuliacha
Kanisa. Kisha umwombee. Ndipo umtembelee na kumwalika arejee katika uhusiano
na Mungu wake kwa njia kumwabudu Mungu kila Juma kwa njia ya mafundisho na
upatanisho katika mahusiano.

Tunakusudia kwamba Juma la Urejeshaji limalizike kwa kishindo kwa njia ya ubatizo
kwa wale walioliacha Kanisa. Kama maandalizi ya Juma hili, watakaokuwa tayari
kumrudia Mungu kwa njia ya ubatizo watiwe moyo na wapewe huduma hii ya
kumrejea Mungu.

Ninawaombea mafanikio makubwa katika maandalizi ya kuwarudisha walioacha


mahusiano na Mungu wao.

Mungu akubariki,

Katibu Mkuu WTC


Mchungaji Azza B. Nyamakababi

nakala Mwenyekiti Jimbo la Magharibi mwa Tanzania


Mhazini Jimbo la Magharibi mwa Tanzania

You might also like